Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TEMS: Mmiliki San Diego anayefuata nyayo za waafrika hawa

Muktasari:

  • Tems ni msanii wa muziki wa AfroBeat mapema wa Nigeria na anakuwa mwanamke wa kwanza kumiliki timu ya Marekani, huku wengine wanaomiliki sehemu nyingine ni Akosua Puni Essien  anayeimiliki FC Como ya Italia, Eniola Aluko anayeimiliki timu ya wanawake ya FC Como na Nneka Ede anayeimiliki Lusitano SAD  ya Ureno.

MWANADADA Temilade Openiyi ‘Tems’ ameungana na nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United na Chelsea, Juan Mata kama sehemu ya wamiliki wa klabu ya soka ya San Diego FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani.

Tems ni msanii wa muziki wa AfroBeat mapema wa Nigeria na anakuwa mwanamke wa kwanza kumiliki timu ya Marekani, huku wengine wanaomiliki sehemu nyingine ni Akosua Puni Essien  anayeimiliki FC Como ya Italia, Eniola Aluko anayeimiliki timu ya wanawake ya FC Como na Nneka Ede anayeimiliki Lusitano SAD  ya Ureno.

Tems ambaye anatamba na kibao cha ‘Get it Right’ aliyomshirikisha Asake ni msanii wa kwanza kuwekeza pesa kwenye timu.

Baada ya kuwa mmoja wa wamiliki, aliandika katika ukurasa wake wa kijamii; “Helo San Diego, ni mimi Tems, na ninafuraha kubwa kuwa sehemu ya SDFC. Nimefurahishwa sana kujiunga na kundi la wamiliki wa San Diego FC na kuwa sehemu ya klabu inayosherehekea ubunifu, utamaduni na jamii. Mpira wa miguu unaunganisha watu kwa njia ya kipekee, na ninatamani kusaidia kujenga kitu maalum hapa San Diego.”

Aliongeza; “Sikuzote nimekuwa nikipenda mpira. Nilipokuwa mdogo, nilikuwa nikimuangalia kaka yangu akicheza na marafiki zake, na kila mara nilivutiwa sana.”


Ana tuzo kadhaa kutokana na muziki wake ikiwamo ile kubwa ya Grammy aliyoshinda Februari mwaka huu katika kipengele kipya ambacho ni maalum kwa muziki wa Afrika cha Best African Music Performance kupitia wimbo wake, Love Me Jeje (2024) na kuwa msanii wa kwanza wa kike Nigeria kushinda Grammy na wa pili baada ya Burna Boy aliyeshinda mwaka 2021.

Rekodi nyingine  ni kuwa msanii wa pili Afrika kushinda kipengele cha Best African Music Performance baada ya Tyla wa Afrika Kusini kushinda mwaka 2024 kupitia wimbo wake maarufu, Water (2023).

Tuzo nyingine ni Best Melodic Rap Performance kupitia wimbo “Wait for U” alioshirikishwa na Future na rapa Drake, BET Awards (2022) kama Best International Act na Best Collaboration kwa wimbo “Essence” na Wizkid na Soul Train Music Awards (2021) katika kipengele cha Best Collaboration kwenye wimbo huo huo.

Utakumbuka Tems alianza kupata umaarufu Nigeria na Afrika baada ya kutoa EP yake ya pili, If Orange Was a Place (2021) yenye nyimbo kali kama ‘Free Mind’ ulioshika nafasi ya kwanza chati za Billboard U.S. Afrobeats Songs na Bubbling Under Hot 100.

Hata hivyo, ukubwa wa jina lake uliongezeka aliposhirikishwa na Wizkid katika wimbo, Essence (2020) uliochaguliwa kuwania Grammy na kushinda BET 2022 kama Wimbo Bora wa Kushiririkiana, huku Tems akishinda kama Msanii Bora wa Kimataifa.

Mbali na tuzo hizo amefanya kolabo na wasanii wakubwa duniani akiwemo Justin Bieber kwenye remix ya wimbo wa Essence, Drake  kwenye wimbo wa ‘Fountains’ (2021), Beyonce ‘Move’ (2022), Rihanna ‘Lift Me Up’ (2022).

Mwanaspoti imekuchambulia baadhi ya wanawake wa Kiafrika waliomiliki timu Ulaya.


1. Akosua Puni Essien (FC Como)

Kwa sasa FC Como inashiriki Ligi Kuu nchini Italia ‘Serie A’ ikiwa nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Akosua Puni Essien ambaye ni mke wa nyota wa zamani wa Chelsea na timu ya Taifa ya Ghana, Michael Essien aliingia kwenye kitabu cha rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza wa Afrika kumiliki timu ya kigeni.

Mwaka 2017 Essien aliinunua Como wakati huo ikishiriki Ligi daraja la tatu nchini humo.

Como ilipitia kipindi kigumu cha kufilisika kutokana na matatizo ya kifedha na viongozi wakalazimika kuiuza ndio mwanamama huyo akaiununua kwa dau la Euro 237,000 (Sh700 milioni) za Kitanzania.

Ilielezwa hilo ndio lilikuwa dau kubwa kuzidi washiriki zaidi ya 30 waliokuwa wanaitaka kununua klabu hiyo.

Ununuzi huo ulimfanya kuwa Mghana wa kwanza kumiliki klabu barani Ulaya na mwanamke wa kwanza wa Kiafrika kufanya hivyo, pia mmiliki wa kwanza mwanamke wa kigeni wa klabu Italia.


2.Nneka Ede (Lusitano SAD)

Baada ya Essien kuinunua klabu ya Italia, miaka mitatu baadae Mnigeria Nneka Ede alikuwa mwanamke wa pili kutoka Afrika kumiliki klabu ya kigeni baada ya kuinunua Lusitano GC FC iliyokuwa inashiriki Ligi daraja la tatu Ureno mwaka 2020.

Hapo awali mwanadada huyo aliwahi kucheza soka la daraja la kati nchini Uingereza ambako alizaliwa na kukulia huko.

Alinunua hisa zote (asilimia 100) za klabu hiyo yenye historia ya zaidi ya miaka mia moja nchini Ureno.

Wakati huo, alisema kuwa lengo lake halikuwa tu kuijenga klabu hiyo, bali pia kusaidia kuunda njia ya maendeleo kwa wachezaji chipukizi.

“Nimefurahishwa na fursa hii na natumaini kuwa sura hii mpya itaendeleza uhusiano mzuri wa michezo uliopo kati ya Nigeria na Ureno, kuendeleza historia tajiri ya klabu ya Lusitano, na kutoa njia kwa vipaji vya vijana kuendelezwa na kung’aa.”

Hadi sasa Ede bado ni mmiliki wa klabu hiyo iliyoko katika jiji la Ãvora, ambayo inashiriki Ligi daraja la tatu.


3. Eniola Aluko (FC Como Women)

Kwa sasa anajishughulisha na uchambuzi wa soka akiwa kwenye vituo mbalimbali kama BBC na Fox Sports.

Mwaka 2024 alinunua timu ya wanawake ya FC Como na kuongeza idadi ya kinadada kutoka Afrika wanaomiliki timu za Ulaya.

Aluko ambaye ni mzaliwa wa Nigeria aliyewahi kucheza soka la kulipwa England na alitangaza ni mmoja wa wawekezaji kwenye klabu hiyo.

Nyota huyo wa zamani wa Chelsea alihamia England na kuwa Mkurugenzi wa Michezo katika klabu ya Aston Villa na Angel City FC za Uingereza.

Akizungumza kuhusu uwekezaji huo, Aluko alisema:

“Tulipata umiliki mkubwa katika FC Como Women; ilikuwa ni hatua ya kujaribu kubadilisha simulizi la soka la wanawake, kuzungumza na hadhira mpya, na kuunda ulimwengu mpya wa soka la wanawake kupitia uwekezaji.”

Baadhi ya timu alizocheza Aluko Uingereza ni Birmingham City msimu 2001/2004, Charlton Athletic 2004/07, Chelsea 2007/09 na Juventus 2018/19.