Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukapteni Taifa Stars apewe Msuva

STARS Pict

Muktasari:

  • Kwanza ieleweke kwamba huu ni ushauri wa kijiwe kwa wachezaji ambao wao ndio watafanya uteuzi wa nani awe kiongozi wao katika Taifa Stars na sio kwamba tunawalazimisha.

KITAMBAA cha ukapteni wa Taifa Stars baada ya Mbwana Samatta kustaafu, kijiwe kinashauri kiende begani kwa Saimon Msuva.

Kwanza ieleweke kwamba huu ni ushauri wa kijiwe kwa wachezaji ambao wao ndio watafanya uteuzi wa nani awe kiongozi wao katika Taifa Stars na sio kwamba tunawalazimisha.

Tunajua wapo wachezaji wengi katika kikosi cha Taifa Stars kilichoitwa sasa hivi ambao wana sifa za kuwa makapteni na yeyote atakayechaguliwa itakuwa freshi tu ila itakuwa vizuri kama watampendekeza Msuva.

Msuva ukikitazama kikosi cha sasa, yeye inawezekana ndio mchezaji aliyeitumikia Taifa Stars kwa muda mrefu zaidi inawezekana ikawa hivyo kwa Himid Mao.

Kingine Msuva anabeba heshima ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi akiwa na kikosi cha Taifa Stars sawa na Mrisho Ngassa kila mmoja akiwa amefunga mabao 25.

Hii inakupa tafsiri kwamba Saimon Msuva ni miongoni mwa wachezaji ambao wanajituma sana pindi wanapokuwa wamevaa jezi na kuitumikia timu ya taifa maana mabao hayawezi kujifunga yenyewe.

Mchezaji kama yeye anapaswa kuheshimishwa pindi mashindano kama AFCON yanapochezwa katika ardhi ya nyumbani kwa kupewa jukumu la kuongoza wenzake.

Kingine jamani tukumbuke Msuva anaelekea katika nyakati za kustaafu kuitumikia Taifa Stars na hana muda mrefu wa kuichezea timu hiyo hivyo anapaswa pale atakapoamua kustaafu basi afanye hivyo akiwa na kitambaa katika bega lake cha ukapteni.

Wengine subirini kidogo nafasi yenu itafika lakini kwa sasa emu nchi tumbebeshe jukumu hilo Saimon Msuva.