Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vyakula vinavyoongeza urembo wako

VYAKULA Pict

Muktasari:

  • Kabla hujafikiria kuongeza bidhaa nyingine kwenye droo yako ya urembo, huenda suluhisho la kwanza liko kwenye glasi ya maji, kipande cha parachichi au sahani ya mboga za majani.

WAKATI wengine wanatumia fedha nyingi kununua vipodozi, mafuta na bidhaa za ngozi wakiamini ndizo siri ya kuonekana vizuri, kuna ukweli mmoja ambao wengi huupuuza  urembo wa asili hauanzi kwenye kioo, unaanzia kwenye sahani yako.

Ngozi inayong’aa, nywele zenye mvuto na kucha zenye afya mara nyingi ni matokeo ya kile unachokunywa na kula kila siku.

Kabla hujafikiria kuongeza bidhaa nyingine kwenye droo yako ya urembo, huenda suluhisho la kwanza liko kwenye glasi ya maji, kipande cha parachichi au sahani ya mboga za majani.

Lishe bora si kwa ajili ya afya tu, bali ni moja ya siri kubwa zinazoweza kubadilisha mwonekano wako bila kutumia gharama kubwa.

VYAKU 03

MAJI MENGI

Miongoni mwa vitu muhimu zaidi vinavyochangia urembo wa asili ni maji. Ingawa watu wengi huyachukulia kawaida, maji yana mchango mkubwa katika kuifanya ngozi ibaki laini, yenye unyevunyevu na kupunguza mwonekano wa uchovu.

Mwili unapokosa maji ya kutosha, ngozi huanza kuonekana kavu, kuchoka na wakati mwingine kupoteza mng’ao wake wa kawaida. Kunywa maji kwa kiwango kinachotosha kila siku husaidia mwili kusafisha sumu na kuruhusu seli kufanya kazi vizuri zaidi.

VYAKU 01

MATUNDA

Mbali na maji, matunda yana nafasi kubwa katika kuongeza uzuri wa asili. Matunda mengi yana vitamini na madini yanayosaidia kurekebisha seli za ngozi na kulinda mwili dhidi ya uharibifu unaosababishwa na mazingira.

Machungwa, mapapai, maembe, nanasi na matunda yenye rangi kali huwa na kiwango kizuri cha vitamini C ambacho husaidia mwili kutengeneza collagen. Hiki ni kirutubisho muhimu kinachosaidia ngozi kubaki yenye uimara na kuchelewesha dalili za kuzeeka mapema.

Tikiti maji pia ni tunda lenye mchango mkubwa kwa sababu lina maji mengi ambayo husaidia mwili kubaki na unyevunyevu wa kutosha huku likiifanya ngozi ionekane safi.

VYAKU 02

MBOGA ZA MAJANI

Mboga za majani nazo ni silaha muhimu katika safari ya kupata urembo wa asili. Mboga kama mchicha, matembele, broccoli na mboga nyingine za kijani zina virutubisho vinavyosaidia ngozi, nywele na kucha.

Mboga hizi huwa na vitamini A ambayo husaidia ngozi kujijenga upya na kupunguza ukavu. Pia zina madini yanayosaidia ukuaji wa nywele na kuimarisha mizizi yake.

Kwa watu wanaokabiliwa na tatizo la nywele kukatika au kupoteza mng’ao wa ngozi, kuongeza mboga kwenye mlo wa kila siku kunaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa muda.

VYAKU 05

USIACHE KULA HIVI

Pia usisahau vyakula vyenye mafuta mazuri. Kuna dhana kwamba mafuta yote ni mabaya, lakini ukweli ni kwamba mwili unahitaji mafuta yenye afya ili kusaidia ngozi kubaki laini na nywele zisiwe kavu.

Parachichi ni mfano mzuri wa chakula kinachosaidia kuongeza urembo wa asili.

Lina mafuta yanayosaidia ngozi kuwa laini na yenye mwonekano wa afya. Karanga na mbegu mbalimbali pia zina mchango mkubwa kwa sababu zina virutubisho vinavyosaidia kujenga seli mpya.

Vyakula vyenye protini ni muhimu sana. Mayai, samaki, maziwa na vyakula vya jamii ya kunde husaidia kuzijenga kucha na kuzifanya zisiwe rahisi kuvunjika.

Mayai pia yana kirutubisho kinachosaidia afya ya nywele na kuifanya ionekane yenye nguvu zaidi. Wataalamu wa lishe pia wanasisitiza umuhimu wa kupunguza matumizi ya sukari nyingi na vyakula vilivyosindikwa kupita kiasi.

Ingawa vinaweza kuonekana havina madhara ya haraka, matumizi ya muda mrefu yanaweza kuathiri ngozi na kuifanya ionekane kuchoka mapema.


KULALA VIZURI

Pamoja na kula vizuri, usingizi wa kutosha na kufanya mazoezi mara kwa mara vina mchango mkubwa katika kuufanya mwili utumie virutubisho vizuri zaidi.