Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tshishimbi: Wiki 2 tosha

NAHODHA wa klabu ya Yanga, Papy Tshishimbi ameweka wazi kwamba wakipewa wiki mbili zitatosha wao kuonyesha ubora wao katika Ligi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Tshishimbi alisema; “Tupo vizuri hakuna ambaye alikuwa anakaa bila kufanya mazoezi, lakini tukipewa wiki mbili tutakuwa bora zaidi ya sasa na tayari kabisa kwa Ligi.”

“Tunaweza kurudi katika ubora wetu kama tuliosimama nao tu, bali wachezaji wanatakiwa kujiamini kwa pamoja,” aliongeza.

Kwa upande wa Ligi kuchezwa sehemu moja, Tshishimbi alisema kwa Dar es Salaam kuna viwanja vizuri kwasababu wachezaji wenzake wa kigeni hawajazoea kucheza viwanja kama vya mkoani.

Yanga wanaendelea kufanya mazoezi katika uwanja wa Chuo cha Sheria, Simu 2000 huku mazoezi hayo yakisimamiwa na kocha msaidizi Charles Mkwasa.