Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chirwa ataja siri ya ubora Geita Gold

CHIRWA Pict

Muktasari:

  • Timu hiyo ilianza msimu kwa kushinda mechi mbili kati ya sita, ukiwamo ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya Kagera Sugar, lakini imekumbana na changamoto kwani sasa imecheza michezo 11 na kukusanya pointi tisa.

GEITA Gold imejikuta katika kipindi kigumu cha matokeo Ligi Kuu Bara, hali inayoiweka kwenye presha ya kurejesha makali iliyokuwa nayo mwanzo wa msimu, lakini mshambuliaji Obrey Chirwa anaamini suluhisho lipo mikononi mwao wenyewe wachezaji.

Timu hiyo ilianza msimu kwa kushinda mechi mbili kati ya sita, ukiwamo ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya Kagera Sugar, lakini imekumbana na changamoto kwani sasa imecheza michezo 11 na kukusanya pointi tisa.

Chirwa ni miongoni mwa wachezaji wenye uzoefu mkubwa katika soka la Tanzania, akiwa amezitumikia timu mbalimbali zikiwemo Yanga, Azam FC, Namungo, KenGold, Ihefu na Kagera Sugar kabla ya kujiunga na Geita Gold.

Mzambia huyo amesema pamoja na matokeo ambayo wamekuwa wakiyapata wachezaji hawajakata tamaa na wanaendelea kujipanga kubadilisha mwenendo huo mara ligi itakaporejea, akisisitiza kuwa nguvu, umoja na msukumo ndio vitakuwa msingi wa kuamka.

CHIRW 01

Chirwa amesema kila mchezaji amekuwa akiumizwa na matokeo wanayopata, hasa kwa kuzingatia kwamba katika baadhi ya michezo wamekuwa wakionyesha kiwango kizuri lakini wanashindwa kukipambanua kwa ushindi.

“Matokeo tunayoyapata yanatuumiza kila mmoja wetu, hakuna mchezaji anayefurahia hali hii. Lakini kinachonifurahisha ni namna ambavyo sisi wenyewe wachezaji tunavyojipanga na kuendelea kuhamasishana ili kutoka kwenye hali hii.

“Tunajua tuna uwezo wa kufanya vizuri zaidi, tunahitaji kuongeza nguvu na msukumo wetu kama wachezaji ili tutakaporejea kwenye ligi tuanze kupata matokeo mazuri na kurejea kwenye njia ya ushindi,” amesema Chirwa.


CHIRW 02

CHIRWA NA GEITA

Chirwa amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu katika kikosi hicho kupitia mabao aliyofunga, ambapo mshambuliaji huyo amefikisha mabao matano katika Ligi Kuu.