Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Familia ya Nditi yazidi kutesa England

FAMILIA ya kiungo wa zamani wa Kikwajuni na timu ya taifa ya Zanzibar, Eric Nditi inaendelea kutesa katika soka la Ulaya baada ya watoto watatu wengine wa staa huyo kuibukia katika timu ya vijana ya Reading iliyo Ligi Daraja la Kwanza, England.

Wakati kaka yao, Adam Nditi akiwa ameingia kikosi cha kwanza cha Chelsea, mdogo wake anayemfuatia, Roberto Nditi (13) yuko katika kikosi cha timu ya Reading chini ya miaka 14, na mapacha wawili (pichani) wanaofuatia, Zion na Paolo (8) wako katika kikosi cha Reading chini ya miaka 10.

Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Basingstoke, Uingereza, Nditi alisema kwamba watoto wake mapacha walitakiwa na Chelsea lakini akashindwa kuwapeleka kwa sababu ya kushindwa kugawanya muda.

“Hawa Zion na Paolo walichukuliwa na Reading ingawa Chelsea iliwataka kwa sababu ningeshindwa kumudu kumpeleka kaka yao Reading kisha niwe nawapeleka wao London. Ndio maana nikaamua wote wakulie Reading,” alisema Nditi.