Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya Ibenge Azam yafikia pazito, vikao havikauki


AZAM FC imeanza harakati za kuhakikisha inambakisha kocha wake, Florent Ibenge, baada ya kuibuka kwa taarifa kuwa ameingia kwenye mchakato wa kuwania nafasi ya ukocha wa timu ya taifa ya Mali.


Ibenge amewasilisha maombi ya kuinoa Mali maarufu kama ‘The Eagles’ na tayari amefanikiwa kuingia kwenye orodha ya mwisho ya makocha wanaowania nafasi hiyo.

Kocha huyo raia wa DR Congo alikuwa katika mchujo huo pamoja na Wareno Antonio Conceicao Oliveira na Anthony Da Silva, Mmorocco Badou Zaki pamoja na kocha mzawa Mohamed Magassouba.

Taarifa kutoka ndani ya Azam FC zinaeleza kuwa uongozi wa klabu hiyo bado una nia ya kuendelea kuwa na Ibenge, jambo lililosababisha kufanyika kwa vikao kati yake na Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Mhispania Octavi Anoro.

Katika kikao hicho, Ibenge alieleza namna ambavyo amekuwa akihitajika na Shirikisho la Soka la Mali, huku Azam ikimhakikishia kuwa bado ina imani naye na inahitaji kuendelea kufanya kazi naye.

“Ibenge amewaambia viongozi kuwa anatamani kubaki Azam, lakini amekiri kuwa Mali imeonyesha nia kubwa ya kumhitaji. Hata hivyo, bado hajafanya maamuzi ya mwisho,” kilisema chanzo hicho.

“Tunataka kuendelea kuwa naye. Ingawa huu ni msimu wake wa kwanza na hatujafanikiwa kutwaa taji, tunaamini mustakabali wa timu yetu ni mzuri ikiwa ataendelea kubaki.”

Chanzo hicho kiliongeza kuwa Azam tayari imekamilisha makubaliano ya kuongeza mkataba wa kocha huyo na kilichobaki ni yeye kuweka saini.

“Tuliingia naye mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mwingine. Tulionyesha nia ya kuendelea naye mapema na tayari tumefikia makubaliano. Kilichobaki ni kusaini tu.”

Ibenge ni mmoja kati ya makocha bora Afrika akiwa amefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya CHAN akiwa na DR Congo, pia akiiwezesha Azam kwa mara ya kwanza kufika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Timu yake kwa sasa ikiwa imepoteza mchezo mmoja tu kwenye ligi ipo nafasi ya tatu na pointi 52 baada ya kucheza michezo 25 ya ligi.