Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kambi yampa mzuka Morocco        

KAMBI Pict

Muktasari:

  • Kwa upande wa Morocco alianza maisha yake vizuri na kikosi hicho, baada ya kupata ushindi wake wa kwanza tangu ajiunge nao wa mabao 3-1, dhidi ya Pamba Jiji, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini, Mwanza, mechi iliyopigwa, Septemba 13, 2026.

KOCHA Mkuu wa TRA United, Hemed Suleiman ‘Morocco’, amesema kambi ya zaidi ya wiki moja iliyoweka kikosi hicho visiwani, Zanzibar imekuwa na matokeo chanya, kwa sababu imejenga utulivu wa wachezaji kujiandaa na mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Mwanaspoti, Morocco amesema kambi hiyo imekuwa na manufaa makubwa katika kipindi hiki cha kupisha kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), ili kufanyia kazi upungufu uliojitokeza kwenye mechi walizocheza hadi sasa.

“Bado hatuna muunganiko mzuri wa kiuchezaji kwa maana ya safu yetu ya kujilinda na ile ya ushambuliaji, tunafunga mabao lakini tunaruhu pia, hiyo ni kazi kubwa tuliyokuwa tunaifanyia mazoezini na maendelezo yetu ni mazuri,” amesema Morocco.

Aidha, Morocco amesema kambi hiyo ya zaidi ya wiki moja iliyoanza visiwani, Zanzibar, tangu Septemba 21, 2026, italeta manufaa chanya, licha ya kukiri ushindani umekuwa ni mkubwa, kutokana na mahitaji ya kila timu kwa msimu wa 2026-2027.

Kocha huyo aliyeifundisha pia timu ya Taifa ya Tanzania na klabu mbalimbali za Bara zikiwemo Simba, Namungo FC na Geita Gold, alijiunga rasmi na TRA United, Septemba 10, 2026, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Mrundi Etienne Ndayiragije.

Ndayiragije aliyejiunga na TRA United, Novemba 16, 2025, akitokea Kenya Police FC ya Kenya, aliyoipa ubingwa wa Ligi Kuu ya Kenya kwa msimu wa 2024-2025, aliachana na kikosi hicho rasmi Septemba 7, 2026, kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Katika mechi tano Ndayiragije alizoiongoza TRA United kwenye Ligi Kuu msimu wa 2026-2027, alitoka sare tatu na kupoteza mbili na kuiacha timu hiyo ikiwa nafasi ya 13 na pointi tatu, huku ikifunga mabao matatu tu na kuruhusu mengine matano.

Kwa upande wa Morocco alianza maisha yake vizuri na kikosi hicho, baada ya kupata ushindi wake wa kwanza tangu ajiunge nao wa mabao 3-1, dhidi ya Pamba Jiji, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini, Mwanza, mechi iliyopigwa, Septemba 13, 2026.