Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha wa Bandari FC aitaka Ligi Kuu Bara

BANDARI Pict

Muktasari:

  • Bandari Tanzania inatarajia kushiriki Championship kwa mara ya kwanza baada ya kufanya vizuri kwenye First League na kwa sasa imeweka kambi yake Mtwara kujiwinda na ligi hiyo kuisaka Ligi Kuu.

WAKATI Bandari Tanzania ikiendelea kujifua kwa ajili ya Championship msimu ujao, kocha mkuu wa timu hiyo, Habibu Kondo amesema matarajio yake ni kuipeleka Ligi Kuu kama alivyowahi kufanya akiwa na Azam FC.

Bandari Tanzania inatarajia kushiriki Championship kwa mara ya kwanza baada ya kufanya vizuri kwenye First League na kwa sasa imeweka kambi yake Mtwara kujiwinda na ligi hiyo kuisaka Ligi Kuu.

Pamoja na maandalizi iliyonayo, matajiri hao wanatamba na usajili bora walioufanya wa mastaa kutoka ndani na nje ya nchi waliowahi kutesa Ligi Kuu wakiwa na timu kubwa nchini akiwamo Joyce Lomalisa aliyewahi kucheza Yanga.

BANDA 01

Pia wamo nyota wenye uzoefu na soka la ushindani wakiwa ni Sixtus Sabilo, Mohamed Kassim, Ally Ramadhan, Razack Shekimweli, William Elias, Seleman Omary ‘Boban’, Hajji Ugando, Issah Ngoah, Ayoub Semtawa na Geofrey Kiggi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kondo amesema usajili walioufanya ni mahitaji ya timu hiyo katika kufikia malengo, na maandalizi waliyonayo yanaonyesha mwanga kutimiza ndoto za kucheza Ligi Kuu.

BANDA 02

Amesema licha ya kuwa na wachezaji wenye majina makubwa, lakini wamezingatia kiwango cha kila mmoja na uzoefu na uwezo wake kwenye soka la ushindani ni kete nyingine kuipeleka timu hiyo Ligi Kuu.

“Hatujaangalia majina tu bali hata ubora wa mchezaji na kiwango chake, naamini kwa mipango yetu na mapenzi ya Mungu tunaweza kupanda Ligi Kuu kwakuwa ninayo historia nikifanya hivyo Azam FC 2008,” amesema Kondo.

Kocha huyo ameongeza wakati wakiendelea kujifua, anatarajia kuwa na mechi kadhaa za kirafiki kwa ajili ya kutengeneza muunganiko, fitinesi na utimamu akicheza na timu zenye ushindani huko Dar es Salaam.

BANDA 03

Amesema anafahamu Championship ugumu wake ikiwamo timu zenye uzoefu wa ligi kama  KMC, Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons na Rhino Rangers nawatakuja na mipango kuhakikisha hawakwami.

“Ndio maana tupo Dar es Salaam kwa ajili ya mechi za kirafiki kuwaweka sawa vijana, tunafahamu ugumu wa ligi hiyo kwakuwa zipo timu zenye uwezo na uzoefu, tutajipanga kufanya kweli,” amesema kocha huyo.