Lipiki achafukwa timu yake kuondolewa

Muktasari:
- Ukonga iliondolewa katika listi kwa bahati mbaya kabla ya kocha huyo kuulizia kwa wahusika na kurejeshwa na kushusha presha mashabiki wa timu hiyo kuhusu ushiriki wao.
Kocha wa Ukonga Queens, Denisi Lipiki amesema timu yake itashiriki Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa Wanawake (WBDL).
Ukonga iliondolewa katika listi kwa bahati mbaya kabla ya kocha huyo kuulizia kwa wahusika na kurejeshwa na kushusha presha mashabiki wa timu hiyo kuhusu ushiriki wao.
Lipiki aliliambia Mwanasposti, baada ya kuuliza, kamishina wa ufundi na mashindano wa ligi ya BDL, Haleluya Kavalambi aliwaeleza timu yake ilisahulika.
“Kwa kweli nilishanga sana timu kuondolewa, hasa ukizingatia imeshiriki ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam zaidi ya miaka nane,” alisema Lipiki.
Timu zilizotangazwa kushiriki ligi hiyo mwaka huu ni Donbosco Lioness, Vijana Queens, JKT Stars, Jeshi Star, Polisi Stars, Tausi Royals, UDSM Queens, DB Troncatti, Pazi Quees na Twalipo Queens.
Baadhi ya wachezaji walioibuliwa na timu hiyo tangu ilipoanzishwa ni Noela Uwandameno, Hafsa Hasan, Neema na Hawa Athumani waliojiunga na Vijana Queens, Judith Nyari, Hellen Simon, Shadya Amir, Kelta Kassim na Jesca Ngisaise( JKT Stars), Monalisa kaijage, Witness Mapunda na Ana Marie (Jeshi Stars).
Wengine ni Winfrida Chikawe, Jacqueline Masinde, Amina Kaswa (Polisi), Gloria Manda (Donbosco Lioness).