Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

M-BET yatumia Sh 226.5 milioni kwa washindi wa Perfect 12

Kampuni ya mchezo ya kubashiri matokeo ya M-BET Tanzania imeendelea 'kumwaga'  fedha kwa washindi  baada ya kumzawadia shabiki wa timu ya Yanga na Chelsea Peter Nangi kitita cha Sh milioni 50.

Nangi ambaye ni mkazi wa Geita, ameshinda kiasi hicho cha fedha  baada ya kubashiri kwa usahihi jumla ya michezo 12 ya mchezo wa kubahatisha wa Perfect12 wa kampuni ya M-Bet Tanzania.

Mkurugenzi Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa Nangi ameibuka mshindi ikiwa siku moja tu baada ya Shabiki wa klabu ya Simba na Arsenal Swalehe Enzi kushinda kitita cha sh 176,470,910 kupitia pia droo ya Perfect12 ya kampuni ya M-Bet Tanzania.

“ M-Bet sasa imeanzisha kampeni mpya inayoitwa ZALI LA M-BET ambapo ukicheza na M-Bet unaweza kujishindia Pikipiki na pesa taslimu kila wiki na mwisho wa kampeni mshindi mmoja ataondoka na Toyota IST,” amesema Mushi.

Kwa upande wake, Nangi amesema kuwa ushindi wake umetokana na kuwa makini katika kuchagua timu bila ya kufauata alama za ushindi ambazo kila timu imekuwa ikipewa katika mkeka.

Amesema alianza kubet miezi sita iliyopita na ushindi huu umempa faraja kubwa sana kwani ataongeza mtaji wake na kujishughulisha zaidi na kilimo.

“Siri kubwa ya kushinda bahati nasibu hii kujua uwezo wa timu pamoja na kufanyia utafiti wa timu, aina ya wachezaji ambao wamesajili, aina ya timu unayocheza nayo pamoja na majeruhi.

Ukibet kwa kupenda timu yako, unapotea kwani lazima uwe mfuatiliaji wa michezo mbalimbali. Kama unajua inafungwa, tabiri hivyo na weka mapenzi pembeni kwenye shughuli hii,” amesema Nangi.