Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majeraha yamtibulia Kachwele Marekani

KACHWELE Pict

Muktasari:

  • Kinda huyo wa timu ya taifa 'Taifa Stars' aliyewahi kupita timu ya vijana ya Azam FC huu ni msimu wake wa pili Marekani na uliopita akiwa na kikosi cha timu ya wachezaji wa akiba ya Whitecaps FC 2 alicheza mechi 20 na kufunga mabao manne.

STRAIKA wa Whitecaps FC anayecheza kwa mkopo Vancouver Whitecaps inayoshiriki Ligi Kuu Marekani (MLS), Cyprian Kachwele amesema msimu huu ameuanza vibaya baada ya kupata majeraha ya nyama za paja.

Kinda huyo wa timu ya taifa 'Taifa Stars' aliyewahi kupita timu ya vijana ya Azam FC huu ni msimu wake wa pili Marekani na uliopita akiwa na kikosi cha timu ya wachezaji wa akiba ya Whitecaps FC 2 alicheza mechi 20 na kufunga mabao manne.

Msimu huu akiitumikia Vancouver, hadi sasa amecheza michezo mitano, akifunga bao moja na asisti moja, baada ya mechi 15 na aliliambia Mwanaspoti alipata majeraha hayo wiki mbili zilizopita baada ya kutoka kwenye majukumu ya timu ya taifa.

"Kabla ya kujiunga na timu ya Taifa, niliumia kwenye mechi nikiwa na timu yangu, sijafikisha mwezi nina kama wiki mbili nauguza majeraha ya nyama za paja," alisema Kachwele na kuongeza;

"Natumai nitarudi haraka uwanjani na kwa sasa nasikilizia majibu ya daktari kujua nitakuwa nje kwa muda gani."

Kachwele alitua Vancouver Whoitecaps na kucheza kikosi cha wachezaji wa akiba Whitecaps FC 2 msimu wa 2023/24 baada ya kuchelewa kufika kutokana na matatizo ya viza na alitokea kikosi cha kwanza cha Azam FC alikocheza mechi tatu nakufunga mabao matatu Ligi Kuu Bara, huku kwenye kombe la FA akiweka wavuni mabao mawili.

Mei 2024, alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na Vancouver dhidi ya Cavalry FC wa Kombe la Canada na kwa kiwango kizuri alichoonyesha katika mechi hizo chache kiliwafanya viongozi wa timu hiyo kumwongezea mkataba.