Makalla: Wanaruangwa ishikilieni Namungo FC

Muktasari:
- Kwa sasa, Namungo inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa imecheza michezo 26 na kukusanya pointi 28.
KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla, amewahimiza wakazi wa Ruangwa mkoani Lindi kuendelea kuiunga mkono timu ya Namungo iliyopo katika Ligi Kuu Bara kwa vile ni kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi wilayani humo.
Akizungumza leo Jumapili, Aprili 13, 2025, na wananchi wilayani Ruangwa, Makalla amesema, uwepo wa timu hiyo katika Ligi Kuu ya NBC umekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha shughuli za kiuchumi.
“Namungo inashiriki Ligi Kuu, ina uwanja hapa. Hii maana yake ni kwamba timu zote za ligi hiyo zinakuja kucheza hapa Ruangwa zikiwamo Simba na Yanga. Hapo ndipo utalii wa kimichezo unapofanyika, hoteli zinapata wateja, mama na baba lishe wanapata wateja nawasafirishaji, hivyo uchumi unakua,” amesema Makalla.
Kwa sasa, Namungo inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa imecheza michezo 26 na kukusanya pointi 28.