Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yachonga njia Afrika, mashabiki kuhusika

Muktasari:

  •  Habari hiyo njema inahusu mambo mawili ambayo ni klabu hiyo kuanza haraka mchakato wa kuandaa utaratibu wa kusafirisha idadi kubwa ya mashabiki kwenda Durban, Afrika Kusini ambako mechi ya marudiano ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch itachezwa Aprili 27 mwaka huu.

KUNA habari zinazoweza kuendeleza furaha ya mashabiki wa Simba baada ya raha waliyonayo ya kuitoa Al Masry ya Misri na kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Jambo lingine ni uwezekano wa kutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mechi ya kwanza Aprili 20, mwaka huu.

 Habari hiyo njema inahusu mambo mawili ambayo ni klabu hiyo kuanza haraka mchakato wa kuandaa utaratibu wa kusafirisha idadi kubwa ya mashabiki kwenda Durban, Afrika Kusini ambako mechi ya marudiano ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch itachezwa Aprili 27 mwaka huu.

Simba imeanza kufanya mawasiliano na mamlaka za kiserikali za Tanzania na Afrika Kusini juu ya masuala ya vibali kwa ajili ya mashabiki kwenda Afrika Kusini ambapo ina hamu ya kuona kundi kubwa linakwenda kwa basi kwa vile hakuna changamoto tofauti na iwapo ingekutana na timu kutoka Kaskazini mwa Afrika ambako ni vigumu kusafiri kwa usafiri wa ardhini.

“Afrika Kusini panafikika na tunatamani kuona mashabiki wetu wengi wanaenda kule na wakiungana na Watanzania wanaoishi huko tutakuwa na namba kubwa ambayo itatufanya tuwe kama tunacheza nyumbani.

“Msimu huu hatutaki mzaha kabisa na mashindano haya maana tunataka kuvuka zaidi ya nusu fainali na Mungu akipenda tuweze kutwaa ubingwa, hivyo kila mchezo tunauchukulia kwa uzito,” alisema mmoja wa viongozi wa Simba.

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally alisema klabu itatoa ufafanuzi juu ya suala hilo.


WASAUZI DAR

Katika hatua nyingine Simba imewatoa wasiwasi mashabiki juu ya matumizi ya Uwanja wa Benjamin Mkapa ambao umefungwa kwa muda ikisema inaendelea na mazungumzo na serikali kujua hatua za marekebisho yanayohitajika kufanyika kabla ya mechi dhidi ya Stellenbosch. “Ni mvua tu ambayo ilileta shida lakini kabla haijanyesha eneo la kuchezea lilikuwa katika hali nzuri, hivyo hadi tarehe ya mechi yetu utakuwa sawa na ndio maana hata CAF wenyewe unaona hawajachukua hatua zozote kwa vile sio changamoto kubwa,” kilifichua chanzo toka Simba.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa alisema  timu ya tathmini imeshaanza kukagua hali ya uwanja na mara itakapomaliza wataeleza kitakachoendelea.