Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makambo mguu sawa Ujerumani

Muktasari:

  • Timu hiyo hadi sasa imecheza mechi tisa ikikusanya pointi 18 na nyota huyo akianza kwenye baadhi ya mechi na kufunga bao moja na assisti moja.

KINDA la FCA Darmstadt ya Ujerumani, Athuman Masumbuko 'Makambo Jr ' amesema ameanza kuzoea Ligi na mazingira ya nchi hiyo ambayo ni maraya kwanza kwake.

Timu hiyo hadi sasa imecheza mechi tisa ikikusanya pointi 18 na nyota huyo akianza kwenye baadhi ya mechi na kufunga bao moja na assisti moja.

Makambo Jr aliliambia Mwanaspoti kuwa alipofika alipata ugumu kidogo ingawa sio sana kwa kuwa aliwahi kucheza Denmark.

Aliongeza kuwa ligi ya nchi hiyo imemfanya aanze kuwa mkomavu kwani bila ya kufanya jambo la ziada uwanjani unaweza kuambulia benchi.

"Ligi ya wenzetu haina utani yaani timu zinaingia uwanjani kushindana kweli kwahiyo kocha anahitaji wenye ukomavu ukijisahau kidogo imekula kwako tupo tunaendelea kupambana na juhudi zetu binafsi," alisema Makambo Jr


MECHI ALIZOCHEZA

SpVgg Neu-Isenburg 1 - 0 FCA Darmstadt

FCA Darmstadt  4 - 2 Rot-Weiss Frankfurt

Beienheim  4 - 5 FCA Darmstadt

GroB-Gerau  0 - 2 FCA Darmstadt

FCA Darmstadt 3 - 0 Kickers Offenbach II