Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manqoba awataja wawili Yanga

YANGA Pict


UNAUONA moto wa kikosi cha Yanga kwa sasa? Vuta picha kwenye ubora huo anaongezeka beki na nahodha msaidizi, Dickson Job na mshambuliaji kijana mwenye kasi, Clement Mzize kule mbele.


Hatua hiyo imemfanya Kocha Mkuu wa Yanga, Manqoba Mngqithi kutoa angalizo ndani ya kikosi hicho akisema wachezaji hao wakipona sawa sawa, ushindani wa namba utaongezeka, hali ambayo itawafanya wachezaji kupambania nafasi kitu ambacho benchi la ufundi wanakihitaji zaidi.


Taarifa kutoka idara ya tiba kwenye kikosi cha Yanga ni kwamba Job na Mzize wamebakiza wiki mbili na ile ya tatu itakayofuata watakuwa uwanjani kuanza kazi, maana yake ni kwamba watakosa mechi mbili pekee za Ligi Kuu Bara kuanzia leo dhidi ya Fountain Gate, kisha inayofuata dhidi ya Geita Gold itakayopigwa Septemba 8, 2026.

Idara hiyo imetoa taarifa kwenda idara ya ufundi, wachezaji hao wawili wanaweza kuanza kucheza aidha kuanzia mechi hiyo dhidi ya Geita wakipewa dakika chache au uhakika zaidi wanaweza kupata muda kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United utakaochezwa Septemba 12, 2026.

Mastaa hao wawili wanaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwenye mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba, itakayochezwa Oktoba 10, 2026 endapo benchi la ufundi la timu hiyo litaamua kuwapa nafasi.

Mzize na Job walikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu wakiwa wanauguza majeraha ya goti, na  wawili hao walifanyiwa upasuaji na kukosa karibu msimu mzima uliopita.

UMAF 02

Wachezaji hao kwa sasa wapo kwenye programu na makocha wa mazoezi ya viungo wakiendelea kujipanga kurudi huku pia wakihusika na mazoezi ya timu kubwa kwa kiasi kidogo ili wasiweze kutonesha majeraha yao.

Akizungumzia hatua ya karibu ya kurejea kwa mastaa hao, kocha wa Yanga, Manqoba Mngqithi aliliambia Mwanaspoti, kwa sasa anasubiri hatua ya kurejea rasmi kwa mastaa hao wawili na kuna jipya litaibuka.

Mngqithi amesema watakaporejea wachezaji hao wataongeza upana zaidi wa machaguo kwenye kikosi chake na hatua ya ushindani mkubwa itatoka kwa wale ambao wanawania nafasi dhidi yao katika timu hiyo.

UMAF 03

“Nilisema awali, tunatamani kuwa na uvumulivu mkubwa ili warudi sawasawa, ni kweli wako karibu kuanza kucheza, kwa sasa wako kwenye ratiba ya mwisho kabisa kabla ya kuanza mazoezi kamili na timu nzima,”   amesema Mngqithi.

“Kila mmoja hapa Tanzania anajua kiwango cha wachezaji hao wawili, ni sehemu ya wachezaji muhimu wa timu yetu, wakirejea kuna ushindani zaidi utaongezeka kwenye nafasi ambazo wanazicheza, watashindana.

“Kwetu sisi makocha ni jambo zuri, tunatamani kuona wachezaji wanashindana hapo ndipo timu bora inapoanzia kutengenezwa, jambo zuri ni kwamba timu itaongeza nguvu kubwa zaidi itakayotokana na ibora wa wachezaji wote.”