Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matano awaweka kikao mabeki Fountain Gate

Matano Pict

Muktasari:

  • Fountain Gate imecheza mechi 24, imeshinda mechi nane, sare nne na vipigo 12 imefunga mabao 28 ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara 43 na kuwa timu iliyoruhusu mabao mengi zaidi hadi sasa kwenye ligi msimu huu.

KOCHA Mkuu wa Fountain Gate, Robert Matano amesema kipigo ilichokipata timu hiyo na kupoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya Singida Black Stars kinaendelea kuiweka kwenye hali mbaya safu yake ya ulinzi kutokana na kukosa umakini na kuruhusu mabao mengi msimu huu huku akipanga kukaa chini na safu hiyo kutaka kufahamu shida ipo wapi.

Fountain Gate imecheza mechi 24 hadi sasa na ndio timu inayoongoza kwa kufungwa mabao mengi zaidi msimu huu ambayo ni 43 ikifuatiwa na KenGold ambayo imefungwa mabao 40 kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Azam FC.

Akizungumza na Mwanaspoti, Matano ambaye alijiunga na Fountain Gate akikabidhiwa mikoba ya Mohamed Muya akiiongoza timu hiyo kwenye mechi nane hadi sasa akishinda mbili sare mbili na vipigo vinne, alisema anaangushwa na safu yake ya ulinzi.

“Timu yangu ina makosa mengi ya safu ya ulinzi, nina kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha nayapunguza, bora timu isifunge lakini pia isiruhusu mabao.

“Kwa upande wetu tumekuwa tukifungwa zaidi ya kufunga hili ni tatizo kubwa, bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zilizobaki ili kuinusuru timu.

“Tulicheza na timu nzuri yenye wachezaji wakubwa, kipigo kwetu ni ishara ya kutuonyesha bado tunahitaji kuboresha kila eneo, bado tuna michezo mingine sita ili kukwepa dhahama kama hii ya leo na kutoka kwenye rekodi mbovu ya kuruhusu mabao kwenye kila mchezo, natakiwa kukaa na walinzi nijue shida ni nini,” alisema Matano.

Matano aliongeza bado ana timu  imara inayoweza kushindana na mpinzani yoyote hivyo kupoteza kwao haijawavunja moyo bali itawafanya kupambana zaidi ya sasa ili kwa pamoja waweze kutimiza malengo yao waliyojiwekea msimu huu na kikosi hicho.

Fountain Gate imecheza mechi 24, imeshinda mechi nane, sare nne na vipigo 12 imefunga mabao 28 ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara 43 na kuwa timu iliyoruhusu mabao mengi zaidi hadi sasa kwenye ligi msimu huu.