Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayele mambo magumu Pyramids

Muktasari:

  • Mayele ambaye msimu uliopita akiwa na Yanga alicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika akiifungia mabao manane, ameitumikia timu yake hiyo mpya kwa dakika 1153, kwenye mechi 16 za mashindano yote.

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, anayekipiga Pyramids FC ya Misri, Fiston Mayele ameshindwa kutamba na timu hiyo baada ya kuondolewa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika akisubiri mechi moja dhidi ya FC Nouadhibou.

Mayele ambaye msimu uliopita akiwa na Yanga alicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika akiifungia mabao manane, ameitumikia timu yake hiyo mpya kwa dakika 1153, kwenye mechi 16 za mashindano yote.

Pyramids ipo kundi A na TP Mazembe DR Congo, Mamelod Sundowns na FC Nouadhibou kwenye mechi tano walizocheza, imeshinda mechi moja na sare moja huku akikubali kichapo cha mechi tatu.

Mayele ambaye amecheza dakika 409, Ligi ya Mabingwa Afrika, amecheza mechi sita hana bao hata moja huku akitoa asisti moja, anasubiri mechi moja tu ya kukamilisha ratiba.

Mshambuliaji huyo kwenye ligi amecheza mechi tisa akitumika dakika 604, amefunga mabao manne hana asisti hata moja, kwenye Kombe la Misri amecheza dakika zote 90, lakini hana bao wala asisti, hivyo inamfanya kucheza dakika 1153 za mashindano yote.

Timu yake hatua ya makundi ilianza na ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya TP Mazembe, suluhu dhidi ya Mamelodi Sundowns ugenini, ilikubali kichapo cha mabao 2-0 kwa FC Nouadhibou na kichapo cha mabao 3-0 na TP Mazembe.

Pyramids ipo nafasi ya mwisho kwenye msimamo baada ya kukusanya pointi nne sawa na FC Nouadhibou huku Mamelodi Sundowns ikiwa kileleni na pointi 10 sawa na TP Mazembe iliyopo nafasi ya pili ambazo zote zimeshafuzu.

Timu ya mshambuliaji huyo kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya tatu ikiwa   imecheza mechi 10 imeshinda sita, imepata sare tatu na kufungwa mchezo mmoja huku ikifunga mabao 13 wakifungwa mabao tisa ikikusanya pointi 21.