Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtibwa Sugar ina dk 90 za kihistoria

MTIBWA Pict

Muktasari:

  • Raundi ya 28 ya Ligi ya Championship itahitimishwa leo kwenye Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita kwa vita kali pia kati ya Geita Gold iliyoshuka daraja msimu uliopita dhidi ya Mbeya City, ambazo timu zote zinawania nafasi ya kucheza Ligi Kuu.

VINARA wa Ligi ya Championship, Mtibwa Sugar wana dakika 90 za kuamua hatma ya kurejea Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao kama watashinda mechi ya leo ugenini dhidi ya Bigman FC kwenye Uwanja wa Ilulu Lindi, kwani watafikisha pointi 69, ambazo hazitafikiwa na timu yoyote.

Iko hivi. Mtibwa ina pointi 66, hivyo ikishinda leo itafikisha 69 na kurejea Ligi Kuu kwa msimu ujao, ikiwa na mechi mbili mkono, kwani Mbeya City iliyopo ya pili kwa pointi 59, hata ikishinda mechi tatu zilizobaki itaishia na 68.

Kwa upande wa Stand United ‘Chama la Wana’ ambao ndio wapinzani wakubwa wa Mbeya City wanaowania nafasi mbili za juu ili kucheza Ligi Kuu msimu ujao, wako nafasi ya tatu na pointi 58, hivyo wakishinda mechi zote tatu wataishia na 67.

Mechi nyingine za raundi ya 28 leo, Cosmopolitan iliyochapwa mabao 2-0 na Biashara United, itaikaribisha Stand United inayopambania kupanda Ligi Kuu, huku ikiwa na kumbukumbu ya kuichapa Green Warriors mabao 5-1, mechi ya mwisho.

Maafande wa Green Warriors watakuwa kwenye Uwanja wa Mabatini Pwani kucheza na Biashara United, huku Transit Camp yenye kumbukumbu ya kushinda mabao 2-1, dhidi ya Mbuni FC, itaikaribisha TMA FC iliyotoka sare ya bao 1-1 na Kiluvya United.

Kiluvya United itakuwa nyumbani kuikaribisha Mbuni FC, huku kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara Mbeya Kwanza iliyochapwa bao 1-0, dhidi ya Mtibwa Sugar itacheza na African Sports iliyopoteza mechi ya mwisho kwa Bigman FC mabao 3-1.

Kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Ruvuma, wenyeji Songea United waliochapwa mabao 2-1 na Geita Gold, watapambana na maafande wa Polisi Tanzania, wenye kumbukumbu mbaya baada ya kuchapwa mchezo wao wa mwisho kwa mabao 4-2 na Mbeya City.

Raundi ya 28 ya Ligi ya Championship itahitimishwa leo kwenye Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita kwa vita kali pia kati ya Geita Gold iliyoshuka daraja msimu uliopita dhidi ya Mbeya City, ambazo timu zote zinawania nafasi ya kucheza Ligi Kuu.

Kocha wa Mtibwa Sugar, Awadh Juma ‘Maniche’, alisema anatambua presha ya mchezo huo kutokana na saikolojia ya wachezaji wa kikosi hicho, ingawa amewataka kucheza kama ilivyokuwa mechi nyingine ili wasitoke nje ya maandalizi waliyoyafanya.

“Shauku ya wachezaji ni kubwa sana kwa ajili ya mchezo huu, nimewaandaa vizuri kisaikolojia kwa sababu Bigman ni timu nzuri na hata mechi ya kwanza walitupa changamoto, kiufupi tumejiandaa kama ilivyo michezo mingine,” alisema Maniche, ambaye mechi ya kwanza waliilaza Bigman 1-0.