Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ofisa Tabibu apiga mkwanja na MBet

Muktasari:

Nasson ilifanikiwa kushinda zaidi ya Sh70 Milioni katika mchezo huo wa kubashiri mechi mbalimbali za soka kutoka katika ligi mbalimbali na alifanya hivyo baada ya kupatia kubashiri sahihi mechi 12 zote kama mchezo wenyewe unavyotaka.

Dar es Salaam. Kampuni ya michezo ya kubashiri ya MBet katika droo yake ya 11 ya mchezo wa (Perfect 12) alishinda Given Nasson Ofisa tabibu wa zahanati ya Kyamalanga iliyopo Bukoba.

Nasson ilifanikiwa kushinda zaidi ya Sh70 Milioni katika mchezo huo wa kubashiri mechi mbalimbali za soka kutoka katika ligi mbalimbali na alifanya hivyo baada ya kupatia kubashiri sahihi mechi 12 zote kama mchezo wenyewe unavyotaka.

“Nawashuku MBet kwa kunipa pesa hii ambayo nilibashiri kwa Sh 1000 mechi 12 ambazo nilipata zote na kupigiwa simu kuwa natakiwa kufika Dar es Salaam katika ofisi zao kuchukua pesa yangu tayari nimeshaingiziwa katika akaunti yangu,” alisema.

“fedha hizi nitakwenda kujenga nyumba yangu, nitafanya biashara na kuisaidia familia yangu na nitaendelea kubashiri naimani nitashinda zaidi ya hapa kwani kabla ya kushinda nilishawahi kubashiri mara 104 na bila kukata tamaa,” alisema Nasson ambaye ni mzaliwa wa Dodoma ila kwa sasa anaishi Kagera.

Ofisa habari wa Mbet, David Malley alisema imewaandalia Watanzania zaidi ya Sh1 Bilioni kwa ajili ya Perfect 12 hasa kwa wakati huu ambapo ligi nyingi zinaendelea.

“Nasson ni mshindi wa pili ndani ya huu mwezi kwani Septemba 8 tulitoa zaidi ya Sh239 Milioni kwa mshindi mwingine kwahiyo Watanzania waendelee kubashiri na kampuni yetu kwani tumekuwa tukitoa pesa haraka na mapema kwa washindi,” alisema Malley.