Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rupia amrithi Challe KenGold FC

RUPIA Pict

Muktasari:

  • Licha ya Hausung FC kucheza Championship kwa mara ya kwanza msimu wa 2025-2026, ila ilirejea tena Ligi Daraja la Kwanza, baada ya kumaliza mkiani mwa nafasi ya 16 na pointi tisa tu, ikishinda mechi tatu, sare tatu na kupoteza 24, kati ya 30.

MABOSI wa KenGold FC wamefikia makubaliano ya kumuajiri aliyekuwa Kocha Mkuu wa Stand United ‘Chama la Wana’, Hussein Rupia, baada ya Jumanne Challe aliyeifundisha msimu wa 2025-2026, kujiunga na Polisi Tanzania akimsaidia Mbwana Makata.

Rupia aliyewahi kuifundisha pia Hausung FC ya mkoani Njombe, amejiunga na kikosi hicho kutoka jijini, Mbeya, huku akiwa na mtihani mkubwa wa kuhakikisha anakirejesha tena katika Ligi Kuu Bara, baada ya kushuka daraja kwa msimu wa 2024-2025.

Akizungumza na Mwanaspoti, Rupia amesema licha ya ugeni wake katika kikosi hicho, ila atahakikisha anapambana kwa lengo la kurejesha heshima ya jijini Mbeya, huku akiomba mashabiki na viongozi wa timu hiyo kumpa sapoti ili kutimiza malengo.

“Ni ugeni wa timu ya KenGold FC ila sio katika Ligi ya Championship, nina uzoefu wa kutosha na sasa ni muda wa kuonyesha hapa nilipo, msimu huu ni mgumu hivyo, ni lazima tuungane kwa pamoja ili kuhakikisha tunatimiza malengo,” amesema Rupia.

Rupia aliipandisha Hausung FC ya Njombe kucheza Championship msimu wa 2025-2026, baada ya kuongoza Ligi Daraja la Kwanza kundi A na pointi 25, msimu wa 2024-2025, ikiungana na mabingwa Gunners FC ya Dodoma, iliyoongoza kundi B na pointi 35.

Licha ya Hausung FC kucheza Championship kwa mara ya kwanza msimu wa 2025-2026, ila ilirejea tena Ligi Daraja la Kwanza, baada ya kumaliza mkiani mwa nafasi ya 16 na pointi tisa tu, ikishinda mechi tatu, sare tatu na kupoteza 24, kati ya 30.