Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu kiungo Simba Queens kutocheza zatajwa

Queens Pict

Muktasari:

  • Ligi Kuu ya Wanawake inakaribia mwisho na kiungo huyo Mnigeria aliyehamia kutoka Yanga Princes ambako alikuwa na nafasi ya kudumu kikosini katika michezo 14 ya ligi hadi sasa hajacheza mchezo wowote na alionekana katika mchezo mmoja tu ambao sio wa ligi.

KIUNGO wa Simba Queens, Saiki Atinuke imefichuyka sababu za kukosa mechi zote za msimu huu hadi sasa ni majeraha na matatizo ya kifamilia.

Ligi Kuu ya Wanawake inakaribia mwisho na kiungo huyo Mnigeria aliyehamia kutoka Yanga Princes ambako alikuwa na nafasi ya kudumu kikosini katika michezo 14 ya ligi hadi sasa hajacheza mchezo wowote na alionekana katika mchezo mmoja tu ambao sio wa ligi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha msaidizi wa Simba, Mussa Mgosi alisema nyota huyo alikuwa na kipindi kigumu cha majeraha na baadae alipatwa na matatizo ya kifamilia yaliyofuatana.

"Mwanzo alicheza mechi moja lakini haikuwa ya ligi, baadae akapata majeraha akakaa nje kidogo, hakutulia vizuri alikumbwa na ishu za kifamilia tukamruhusu kwa hiyo alikuwa na mambo mengi na hata aliporudi mechi zilikuwa ngumu zimeingiliana na kocha alikuwa anaangalia wale waliokuwa wanacheza," alisema Mgosi na kuongeza;

"Kwa sasa yuko na timu anaendelea na mazoezi na kocha akiona yuko fiti basi atacheza mechi zilizosalia."

Kwenye kikosi cha Simba waliosajiliwa msimu huu ni Saiki pekee ndiye hajacheza mchezo wowote wa ligi, huku Zawadi Hamis, Josephine Julius, Janet Mpeni, Emiliana Mdimu na Wilfrida Cedar wakicheza kwenye baadhi ya mechi.