Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Santos arejea uwanjani, aitaka Stars

SANTOS Pict

Muktasari:

  • Santos (21) alipata jeraha hilo mwishoni mwa msimu uliopita na kulazimika kufanyiwa operesheni Agosti 8 mwaka huu, jambo lililomweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
  • Akizungumza na Mwanaspoti, Santos amesema kwa sasa amerejea kikosini na yuko tayari kuanza kupambana tena baada ya kipindi kigumu cha kukaa nje kutokana na majeraha. 

MSHAMBULIAJI wa Tanzania, Fahmar Santos amerejea rasmi uwanjani baada ya kukaa nje kwa takribani msimu mzima akiuguza jeraha la goti, huku sasa akiwa na shauku ya kuanza upya safari yake ya soka akiwa na Ciutat Meridiana FC ya Hispania inayoshiriki Ligi daraja la nne maarufu Catalunya.

Santos (21) alipata jeraha hilo mwishoni mwa msimu uliopita na kulazimika kufanyiwa operesheni Agosti 8 mwaka huu, jambo lililomweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Santos amesema kwa sasa amerejea kikosini na yuko tayari kuanza kupambana tena baada ya kipindi kigumu cha kukaa nje kutokana na majeraha. Amesema kurejea kwake ni hatua muhimu kwake na anataka kutumia msimu huu kurejesha kiwango chake.

SANTO 01

Santos amesema moja ya malengo yake makubwa msimu huu ni kufanya vizuri katika klabu ili kupata nafasi ya kuitwa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania, jambo ambalo amesema ni ndoto yake kubwa katika soka.

Mshambuliaji huyo anaingia msimu huu akiwa na kumbukumbu nzuri ya msimu uliopita, ambako alifunga mabao 15 katika mechi 20, kabla ya jeraha kumuweka nje kwa kipindi kirefu. Rekodi hiyo ndiyo inayompa matumaini ya kurejea na kuendelea kuwa tishio kwenye safu ya ushambuliaji.

SANTO 02

Santos amesema kipindi ambacho alikuwa akiuguza jeraha, timu hiyo iliendelea na mapambano ya kutafuta nafasi ya kupanda daraja kupitia play-off, lakini haikufanikiwa baada ya kupoteza michezo ya mwisho.

“Kipindi mimi naumwa timu ilicheza play-off kupanda daraja lakini tukashindwa kupanda, tukafungwa kwa hiyo nimerejea na ninaamini kwa uwezo wa Mungu tutafanikisha malengo ya timu na mimi mwenyewe binafsi,” amesema Santos.

Kiungo huyo alijiunga na timu hiyo msimu wa 2022/23 akitokea Ruvu Shooting aliyoitumikia kwa misimu miwili 2019/20 na 2020/21 na Zanzibar alicheza katika akademi ya Deal Kids.