Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti Boys yazoa tuzo, ikipoteza fainali AFCON kwa Senegal

Muktasari:

  • Hata hivyo, licha ya kupoteza mechi hiyo ya fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Prince Moulay Hassan, Rabat, Serengeti Boys imeongoza kwa kutwaa tuzo nyingi kulinganisha na timu nyingine shiriki.

Matumaini ya Serengeti Boys kutwaa ubingwa wa AFCON U17 yamezimwa katika mchezo wa fainali jana jijini Rabat, Morocco baada ya kupoteza kwa mikwaju ya penalti 4-2 mbele ya Senegal.

Hata hivyo, licha ya kupoteza mechi hiyo ya fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Prince Moulay Hassan, Rabat, Serengeti Boys imeongoza kwa kutwaa tuzo nyingi kulinganisha na timu nyingine shiriki.

Mwanzo wa Serengeti Boys katika mechi hiyo ya fainali awali ulionekana kutia matumaini baada ya kupata bao la kuongoza katika dakika ya saba kupitia kwa Hamis Mihambo aliyemalizia kwa shuti la wastani pasi ya Luqman Mbalasalu.

Hata hivyo Senegal ilisawazisha katika dakika ya 64 kupitia kwa Ibrahima Dione aliyefunga kwa kumalizia mpira uliotemwa na kipa wa Serengeti Boys, Haji Abdallah.

Baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika, mikwaju ya penalti ilitumika kuamua bingwa wa mashindano hayo ndipo Senegal ikapata ushindi wa mikwaju ya penalti 4-3.

Hata hivyo pamoja na kumaliza katika nafasi ya pili, Serengeti Boys imeongoza kwa kutwaa tuzo nyingi katika mashindano hayo.

Athanas Adam wa Serengeti Boys ameibuka kinara wa kufumania nyavu akimaliza mashindano hayo huku akiwa amepachika mabao matatu.

Serengeti Boys yenyewe imeibuka mshindi wa tuzo ya Timu yenye Nidhamu katika Fainali za AFCON U17 2026.

Serengeti Boys pia imetoa mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano ambayo imeenda kwa kiungo Issa Chole na pia imetwaa tuzo ya timu yenye nidhamu

Senegal nao wamefanikiwa kupata tuzo moja binafsi ambayo ni ya Kipa Bora aliyopata mlinda mlango wao, Assane Sarr.

Kwa kutwaa ubingwa wa AFCON U17, Senegal imejihakikishia kitita cha Dola 125,000 (Sh327 milioni) huku Serengeti Boys ikiwa na uhakika wa kupata Dola 90,000 (Sh235 milioni).