Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida yapanga kumrudisha Nouma, Imoro Yanga

Muktasari:

  • Nouma anayecheza TRA United aliyojiunga nayo dirisha dogo la Januari 2026, ni miongoni mwa majina yanayowindwa Singida Black Stars kwa msimu ujao, ingawa ikiwa dili hilo litatiki basi huenda Imoro akaondoka kikosini huku Yanga ikihusishwa kumuhitaji.

WAKATI msimu wa 2025-2026, ukienda ukingoni, tayari kuna vita ya usajili imeanza mapema kwa timu mbalimbali, moja ya majina yanayotwa kutikisa usajili huo ni mabeki Valentin Nouma na Ibrahim Imoro.

Nouma anayecheza TRA United aliyojiunga nayo dirisha dogo la Januari 2026, ni miongoni mwa majina yanayowindwa Singida Black Stars kwa msimu ujao, ingawa ikiwa dili hilo litatiki basi huenda Imoro akaondoka kikosini huku Yanga ikihusishwa kumuhitaji.

Chanzo kutoka ndani ya uongozi wa Singida, kimeliambia Mwanaspoti Nouma anayehusishwa na kurudi Simba baada ya hapo mwanzoni kuondoka, ni chaguo lao msimu ujao katika upande wa beki wa kushoto, jambo linaloweza kumfungulia mlango Imoro.

Nouma alijiunga na Simba, Julai 7, 2024, akitokea FC Saint Eloi Lupopo ya DR Congo kwa mkataba wa miaka mitatu, lakini alifikia makubaliano ya kutoendelea na timu hiyo Julai 12, 2025, kutokana na kutopata nafasi ya kucheza kikosini.

Sababu za kusitisha mkataba na Simba ni baada ya kushindwa kupata namba mbele ya aliyekuwa nahodha wa kikosi hicho, Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr', ambaye pia ameondoka na kujiunga na Yanga.

Beki huyo amekuwa chaguo la kwanza TRA United chini ya Kocha, Mrundi Etienne Ndayiragije mkataba wake na TRA United unafikia tamati mwisho wa msimu huu wa 2025-2026, huku Singida ikipambana kwa ajili ya kuipata saini yake, jambo linaloweza kumwachia Imoro anayehusishwa na Yanga.