Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uhamiaji yapokea Sh2 milioni kuongeza hamasa

Muktasari:

  • Fedha hizo ni ahadi ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Zanzibar, Hassan Ali Hassan ya kununua bao kila mechi kwa lengo la kuwapa hamasa wachezaji wa timu hiyo kuendelea kujituma na kufanya vizuri Ligi Kuu Zanzibar.

TIMU ya Uhamiaji Zanzibar, imepokea Sh2 milioni kutoka kwa Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji ambaye ni Mwenyekiti wa timu hiyo, Ali Juma Abdulkadir ikiwa ni kuongeza hamasa baada ya kufunga mabao kumi kwenye mechi tano za Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) msimu huu.


Fedha hizo ni ahadi ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Zanzibar, Hassan Ali Hassan ya kununua bao kila mechi kwa lengo la kuwapa hamasa wachezaji wa timu hiyo kuendelea kujituma na kufanya vizuri Ligi Kuu Zanzibar.

Mwenyekiti huyo alikabidhi zawadi hiyo Septemba 24, 2026, kwa niaba ya Kamishna Mkuu, Hassan Ali Hassan baada ya kumalizika kwa mechi ya ZPL ambapo Uhamiaji iliichapa Raskazone bao 1-0. Abdulkadir amesema: “Tunafanya hivi kuongeza juhudi na hamasa kwa wachezaji wetu pamoja na benchi la ufundi kufikia malengo ya timu hiyo bila kuchoka.”

Naye, Nahodha wa Uhamiaji, Ahmed Ali ‘Salula’ amemshukuru kiongozi huyo pamoja na wadau wa timu hiyo kwa kuwa bega kwa bega katika kutoa hamasa na michango yao.

Nahodha huyo, amewaomba viongozi hao wasiishie hapo badala yake waendelea na hamasa hizo na kuahidi kuwa hawatawaangusha.

Uhamiaji imeshacheza mechi tano za Ligi Kuu Zanzibar na kushinda zote, ikifunga mabao kumi na kuruhusu moja ikikusanya pointi 15 ikiendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.