Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Umafia wa kocha Yanga wafichuliwa!

UMAFIA Pict


UMEKUWA ukisikia namna Kocha wa Yanga, Manqoba Mngqithi anavyoichambua timu pinzani kuanzia kocha, wachezaji wake na namna timu hiyo inayocheza kwenye mikutano kabla ya mechi  na baada? Sasa kocha huyo amefunguka wapi anapata taarifa hizo.


Iko hivi, katika kila mchezo ambao Manqoba amekuwa akienda kuucheza, ule mkutano wa makocha kuzungumzia mipango ya mechi hiyo inayofuata, kocha huyo amekuwa akishtua kwa namna anavyoichambua kwa kina timu pinzani kuanzia wachezaji wake na namna inavyocheza, nani ni mchezaji hatari, kocha wao anatumia mbinu gani, wanatumia aina gani ya uchezaji, lakini kinachoshtua zaidi ni kuwataja wachezaji kwa majina yao yote matatu bila kusoma sehemu yoyote akiwa hana zaidi ya miezi miwili tangu alipotua hapa nchini akitokea Afrika Kusini.


Hatua hiyo imekuwa ikishtua watu wa soka wakiona kama ni kitu ambacho anakifahamu zaidi hali ya kuwa hana  muda mrefu wa kuweza kuyafahamu hayo yote akiwa ameshacheza michezo minne tu tangu alipoichapa Simba bao 1-0 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii pamoja na ushindi kwenye michezo mitatu ya Ligi Kuu Bara.

UMAF 01

Akizungumza na Mwanaspoti, Manqoba mmoja kati ya makocha wenye misimamo mikali amefafanua sio kwamba ana bahatisha, lakini katika kila mechi ambayo anakwenda kuicheza amekuwa akifanya kazi ya kuangalia mechi zisizopungua tatu zilizopita za kila timu anayokwenda kukutana nayo.

Manqoba amesema katika mechi hizo ndizo zimekuwa zikimpa nafasi ya kuwajua wachezaji, makocha na falisafa za timu pinzani na kwenda kuzifanyia kazi katika kuhakikisha timu yake inafanikiwa kwa kupata ushindi wanaoutaka.

UMAF 02

“Nimeona mmekuwa mkishangaa, unajua kazi yetu kama makocha tuna jukumu muhimu la kujua ubora wa wapinzani, mimi kawaida unapoona nakwenda kucheza na timu fulani basi kabla ya hapo huwa nahakikisha napata mechi zao zisizopungua tatu, naziangalia na kujua ubora na mapungufu yao,” amesema Manqoba.

“Ndani ya hizo mechi ndio napata nafasi ya kujua kila kitu ambacho mnaona nakiongelea, nadhani uliona niliongea kabla ya mechi ya JKT lakini kocha wao Hamad akaona abadilishe mpango kidogo lakini huwezi kubadilisha kila kitu kwa kuwa muda ni mchache ndiyo maana tumefanikiwa.”

UMAF 03

Aidha mbali na kazi hiyo Manqoba amewasifia wachambuzi wake wawili wa mikanda ya video za mechi, akisema nao wamekuwa wakimwongezea kitu katika taarifa ambazo wanazileta kutoka kwenye utekelezaji wa majukumu hayo.

“Nina watu wawili hapa wa kuchambua mikanda ya video, nao naweza kusema ni sehemu ya kazi hii bora wao wanafanya majukumu yao na wanapokuja wanakutana na yale ambayo mimi nayajua kisha tunakuwa tumepata kitu kimoja kilichokamilika kwa usahihi.

“Tunafanya hivi kwenye kila mechi ambazo tutacheza hapa kwenye ligi, ni makosa makubwa kwenda kwenye mechi hujaijua timu na ubora wake, wachezaji wake na kocha wake kwenye ligi nafikiri nimemaliza timu chache sana, hizo nikishamaliza nitakuwa kwenye sehemu nzuri ya kuiona kazi yangu ikoje,”  amesema kocha huyo wa zamani wa Mamelodi Soundowns

Kwenye mechi nne ambazo Manqoba ameshacheza hadi sasa kuanzia dabi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, ameshinda zote huku timu hiyo ikitawala vizuri michezo hiyo ikifunga jumla ya mabao 13 na kuruhusu mawili pekee.