Mount Uluguru Rally yawaita madereva Morogoro

Muktasari:
- Ngorongoro Heroes inashiriki AFCON U20 2025 baada ya kuchukua ubingwa wa mashindano ya kuwania kufuzu kupitia kanda ya baraza la vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
MADEREVA wa mbio za magari watakuwa mkoani Morogoro wiki ya Pasaka kushiriki mashindano wa mbio fupi zitakazobeba bango la Mount Uluguru Rally Sprint.
Mashindano haya yanatarajiwa kushirikisha madereva kutoka Dar es Salaam, Tanga, Arusha na Iringa na yatachezwa tarehe 21 mwezi Aprili mwaka huu kwa mujbu wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mbio za Magari cha Mt Uluguru, Gwakisa Mahigi.
“Tunategemea kuwa na zaidi ya washiriki 30 hadi kufikia siku ya mashindano Aprili 21 mwaka huu,” alieleza Mahigi.
Kivutio kikubwa cha michuano hii ni mkongwe Samir Shanto ambaye amekuwa akishiriki mbio za magari kwa zaidi ya miongo mitatu sasa.
Shanto ambaye ataingia na gari aina ya Ford Proto, amepania kuwaonyesha vijana yeye bado ni bora katika vita ya injini.
“Sijapoteza uwezo wangu na uzoefu wangu ndiyo utawathibitishia vijana mimi ni nani katika mchezo wa mbio za magari nchini,” aliema Shanto, huku dereva mwingine tegemeo kwa mkoa huo wa Morogoro akiwa ni Waleed Nahdi ambaye atacheza na gari aina ya Subaru Impreza N11.
“Niko tayari na nimejiandaa vyema,” alitamba Nahdi.
Kahigi alisema hadi kufikia mwishoni mwa juma madereva 15 walithibitisha kushiriki wakitokea mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Tanga na raundi hii ya mbio fupi inakwenda Morogoro baada ya kutamatika kwa raundi mbili za awali zilizochezwa viwanja vya Tanganyika Packers, jijini Dar es Salaam Januari na Machi mwaka huu.
Sheria za mbio za magari, kwa mujibu wa chama kinachosimamia mchezo huu nchini,AAT, huruhusu magari maalum ya mashindano(homologated cars), pia magari ya kawaida yataruhusiwa endapo yatatimiza vigezo vyote vya usalama kutokana na miongozo ya chama kinachosimamia mchezo huo duniani, FIA.