Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wapinzani wa Simba, Ligi ya Mabingwa Afrika hadharani 

Muktasari:

  • Simba itakutana na 15 de Agosto ya Guinea ya Ikweta katika raundi ya pili ya mchujo wa Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Timu ya FC 15 de Agosto ya Guinea ya Ikweta imefanikiwa kutinga hatua ya pili ya mchujo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo sasa itakutana na Simba.

15 de Agosto imefuzu baada ya kuiondoa Fomboni FC ya Comoro kwa jumla ya mabao 5-0 katika michezo miwili.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Guinea ya Ikweta, 15 de Agosto ilishinda mabao 4-0, kisha kushinda tena mchezo wa marudiano kwa bao 1-0 ugenini na kukamilisha ushindi wa jumla wa mabao 5-0.

Baada ya kuvuka hatua hiyo, timu hiyo sasa inakabiliwa na mtihani mwingine dhidi ya Simba, ambayo iliingia hatua hii baada ya kuiondoa Mighty Wanderers ya Malawi kwa jumla ya mabao 7-1.

Mchezo wa kwanza kati ya 15 de Agosto na Simba umepangwa kuchezwa kati ya Oktoba 16 na 18, huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kufanyika wiki moja baadaye.

Simba, itaanza safari hiyo kwa kucheza mchezo wa kwanza ugenini kisha kurejea Dar es Salaam kwa mchezo wa marudiano.

Mshindi wa hatua hiyo ataingia katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Sababu mechi kuchelewa kuchezwa 

Fomboni FC inatoka Mohéli, moja ya visiwa vinavyounda nchi ya Comoro hivyo safari yake kwenda Guinea ya Ikweta kwa ajili ya mchezo wa ugenini ilihitaji maandalizi ya ziada ya usafiri.

Kwa klabu zenye uwezo mdogo wa kifedha, safari za aina hiyo zinaweza kuhusisha mabadiliko ya ndege, njia nyingi za usafiri na taratibu za uhamiaji.

Kwa mujibu wa mtazamo huo, uamuzi wa kusogeza mbele muda wa mchezo uliipa Fomboni nafasi ya kukamilisha maandalizi yao bila kukumbwa na matatizo ya kiutawala au usafiri ambayo yangeweza kuathiri mchezo.