Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Jr: Ligi ya Kenya sawa na bara

WAZIRI Pict

Muktasari:

  • Kuungana kwake na Kocha Moallin kunatajwa kuwa chachu ya mafanikio kwa nyota huyo, kwani kocha huyo raia wa Marekani mwenye asili ya Somalia amekuwa akiamini uwezo na uzoefu wake katika kuongeza nguvu na ukali kwenye safu ya ushambuliaji ya Mombasa United.

MSHAMBULIAJI Mtanzania, Waziri Junior Shentembo anayekipiga Mombasa United ya Ligi Kuu Kenya amesema ligi ya nchi hiyo haina tofauti kubwa na ya nyumbani Tanzania.

Waziri Junior, ambaye amejiunga na klabu hiyo inayofundishwa na aliyekuwa kocha wa zamani wa Azam FC na Yanga, Abdihamid Moallin, ameweka wazi malengo yake ya kuonyesha ubora wa kufumania nyavu na kuacha alama kubwa kwenye ligi hiyo.

WAZI 01

Akizungumza baada ya kuanza maisha hayo mapya na kuisaidia timu hiyo kupata ushindi mbele ya Kariobangi Sharks, Waziri amesema: “Natamani na huku niweke ufalme pia, naamini ni wakati wa kuonyesha ubora ndani ya ligi ya Kenya.”

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Dodoma Jini ameongeza, mpira wa miguu hauhitaji maneno mengi zaidi ya vitendo uwanjani na amejipanga kuhakikisha anakuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Mombasa United chini ya Kocha Moallin.

WAZI 02

Usajili wa Waziri Junior Kenya unakuja baada ya kupita kwenye klabu mbalimbali za Ligi Kuu Bara zikiwemo Yanga, Azam FC, KMC, na Dodoma Jiji, pamoja na kupata uzoefu wa soka la kimataifa alipokipiga katika Ligi ya Iraq kwenye klabu ya Al-Minaa.

Katika msimu wa 2023-2024 akiwa na KMC, Waziri alikuwa na kiwango bora alipomaliza msimu na mabao 12 na kuwa mshambuliaji pekee kwenye ligi aliyemaliza na mabao mengi, akishika nafasi ya tatu kwenye chati ya wafungaji bora nyuma ya Feisal Salum ‘Fei Toto’ (mabao 19) na Stephane Aziz Ki aliyekuwa mfungaji bora na mabao 21.

WAZI 03

Kuungana kwake na Kocha Moallin kunatajwa kuwa chachu ya mafanikio kwa nyota huyo, kwani kocha huyo raia wa Marekani mwenye asili ya Somalia amekuwa akiamini uwezo na uzoefu wake katika kuongeza nguvu na ukali kwenye safu ya ushambuliaji ya Mombasa United.