Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

WPL vita ya ubingwa bado mbichi

WPL Pict

Muktasari:

  • Vita ya ubingwa kwa WPL iko kwa timu mbili tu Simba na JKT Queens zilizopishana pointi chache kama ilivyo Ligi Kuu Bara ambayo vita inaonekana ipo kwa Simba na Yanga.

KAMA ulikuwa unajua bingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) amepatikana mapema basi mambo bado kabisa.

Vita ya ubingwa kwa WPL iko kwa timu mbili tu Simba na JKT Queens zilizopishana pointi chache kama ilivyo Ligi Kuu Bara ambayo vita inaonekana ipo kwa Simba na Yanga.

Zimesalia mechi nne na tatu kwa baadhi ya timu ili kuamuliwa bingwa wa msimu huu atakayeliwakilisha taifa kimataifa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

JKT iko kileleni na pointi 38 tofauti ya pointi moja na Simba iliyopo nafasi ya pili ikiwa nazo 37 na ndizo zilizoshikilia usukani wa kombe hilo linalotetewa na Simba na haijapoteza mchezo wowote kati ya 18 iliyocheza.

Timu hizi zitakutana Aprili 29, kwenye Uwanja wa KMC Complex  (raundi ya 15) na mchezo wa kwanza uliopigwa uwanjani hapo zilitoshana nguvu kwa sare ya 1-1 na mchezo huo moja ikishanda huenda ikamweka pazuri kwenye kuukaribia ubingwa.