Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga, KVZ kazi ipo Kombe la Muungano

YANGA Pict

Muktasari:

  • Yanga inavaana na KVZ kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba kuanzia saa 1:15 usiku ikiwa ni mechi ya robo fainali na mshindi atasonga mbele kuingia nusu fainali ambapo JKU ilitangulia mapema juzi kwa kuifunga Singida Black Stars na jana zilipigwa mechi nyingine mbili za kuamua kwenda hatua hiyo.

BAADA ya Singida Black Stars kuenguliwa na JKU kwa penalti 6-5 leo itakuwa ni zamu ya Yanga kuvaana na KVZ katika mechi ya michuno ya Kombe la Muungano 2025, ikikumbushia mechi mbili za Kombe la Mapinduzi zilizochezwa mjini Unguja 2019 na 2024.

Yanga inavaana na KVZ kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba kuanzia saa 1:15 usiku ikiwa ni mechi ya robo fainali na mshindi atasonga mbele kuingia nusu fainali ambapo JKU ilitangulia mapema juzi kwa kuifunga Singida Black Stars na jana zilipigwa mechi nyingine mbili za kuamua kwenda hatua hiyo.

Yanga iliyochomoa kushiriki michuano ya msimu uliopita kutokana na kubanwa na ratiba, tayari ipo visiwani humo kwa mchezo huo, huku ikiwa na rekodi nzuri kulinganisha na wapinzani wao hao kwani katika mechi mbili za hivi karibuni za Mapinduzi imeshinda moja na nyingine kuisha kwa suluhu.

Wababe hao wa Bara wanaivaa KVZ ikiwa ni siku chache wakitoka kuinyoa Fountain Gate kwa mabao 4-0, ikiwa ni mechi ya 23 kucheza bila kupoteza tangu Desemba 7, mwaka jana walipopoteza mechi ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mbele ya MC Alger ya Algeria.

Katika mchezo huo, Yanga inasaka rekodi ya Simba kutwaa taji hilo baada ya kurejea tena msimu uliopita, huku KVZ ikisaka rekodi ya kuchukua ubingwa wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza, kwani haijawahi kufanya hivyo tangu ilipoanza kuchezwa mwaka 1982.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha wa Yanga, Hamdi Miloud alisema michuano hiyo ni sehemu ya kuendelea kuimarisha timu na wanaitumia kuhakikisha wachezaji wanakuwa kwenye nafasi nzuri kumalizia msimu pamoja na Kombe la Shirikisho.

“Sio ratiba rahisi kwetu, lakini haiondoi umuhimu wa michuano hii katika kujenga na kuimarisha kikosi changu. Naamini tutatumia mashindano haya kujiweka fiti lakini pia kuhakikisha tunatwaa taji kujenga heshima ya ubora tulionao... naamini kwa kikosi tulichonacho tunaweza kufanikisha azma yetu,” alisema.

Alisema licha ya kuwa na ratiba ngumu ana imani kubwa na kikosi alichosafiri nacho na wachezaji wake watawekeza juhudi kuhakikisha wanatwaa taji hilo na kurudi kumalizia mataji mengine yote wanayoyashiriki.

Kocha Mkuu wa KVZ, Ali Khalid Omar alisema kikosi kipo tayari kwa ajili ya kupambania nafasi ya kutinga hatua inayofuata na kwamba wataingia katika mchezo kwa kuiheshimu Yanga huku malengo yakiwa ni kuhakikisha wanacheza fainali na hatimaye kutwaa taji.

“Kiujumla wachezaji wote wapo katika utimamu mzuri tayari kwa mchezo huo ambao kwetu ni kama fainali kwani tunakutana na timu bora. Tumeibeba michuano hii kama sehemu ya maandalizi, lakini tunataka taji kwa sababu ndio kitu kinawaniwa,” alisema Omar.

Mshindi wa mchezo huo wa leo ataavana na yule wa mechi ya jana iliyozikutanisha kati ya Zimamoto na Coastal Union, huku JKU ilikuwa ikisikilizia mshindi wa mechi ya jana usiku kati ya KMKM na Azam.

Huu ni msimu wa pili kufanyika kwa Kombe la Muungano baada ya kurudishwa tena tangu lilipochezwa mara ya mwisho mwaka 2002 ikifahamika kwa jina la Ligi Kuu ya Muungano iliyokuwa na lengo la kudumisha Muungano wa nchi za Tanganyika na Zanzibar uliosababisha  kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na leo ikiwa ni miaka 61 tangu tukio hilo lilipofanyika Aprili 26, 1964. Msimu uliopita Simba ilitwaa taji kwa kuifunga Azam.