Yanga Princess yamwinda kocha wa timu za taifa
Muktasari:
- Taarifa hizo zinaeleza kuwa uongozi wa timu hiyo umeanza kutazama uwezekano wa kumpata kocha huyo, huku kikosi hicho kikiendelea na maandalizi chini ya kocha Said Maulid, maarufu SMG, anayekaimu nafasi hiyo kwa sasa.
YANGA Princess inaelezwa imeanza mazungumzo na kocha Hilda Masanche ambaye ni mmoja wa benchi la ufundi la timu za taifa za wanawake, ili kuja kurithi mikoba ya Edna Lema aliyeondoka kikosini hapo hivi karibuni.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa uongozi wa timu hiyo umeanza kutazama uwezekano wa kumpata kocha huyo, huku kikosi hicho kikiendelea na maandalizi chini ya kocha Said Maulid, maarufu SMG, anayekaimu nafasi hiyo kwa sasa.
Hata hivyo, mazungumzo hayo bado hayajakamilika kwani awali timu hiyo ilizungumza na Martin Hammel ambaye aliweka ofa kubwa.
“Bado kuna mazungumzo yanaendelea kwa makocha wote wawili, lakini Yanga tageti yake ni Hammel ambaye wanaamini tayari ana uzoefu alioupata akiwa na Tausi lakini pia ana mbinu nzuri lakini pia bado wanamtazama Hilda endapo Hammel hatakubaliana na dili hilo.”
Hilda si jina geni katika soka la wanawake nchini, kwani amekuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu za taifa za wana wake katika ngazi mbalimbali. Uzoefu wake unatajwa kuwa miongoni mwa mambo yanayoweza kumuweka kwenye nafasi ya kuwania jukumu hilo iwapo mazungumzo yatafikia maku baliano.
Hilda aliwahi kufanya kazi na vikosi vya vijana vya wanawake, ikiwamo U-15 kama kocha mkuu na U-17 pamoja na U-20 kama msaidizi wa Bakari Shime katika mfumo wa timu za taifa. Pia, alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la Tanzanite Queens katika Fainali za Kombe la Dunia za Wanawake chini ya miaka 20 zilizofanyika Poland mwaka 2026.