Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha wa zamani Kenya afariki kwa shambulio la moyo

Muktasari:

  • Firat amewahi kuzifundisha pia timu za taifa za Moldova na Iran kwa nyakati tofauti.

Kocha Mkuu wa zamani wa timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’, Engin Firat ameaga dunia leo Jumatatu, Machi 9, 2026 nchini Uturuki kutokana na shambulio la moyo.

Firat mwenye umri wa miaka 55, amefariki muda mfupi baada ya kuanguka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Istanbul, Uturuki wakati alipokuwa akisubiri kuunganisha ndege kwenye mji wa Adana uliopo nchini humo akitokea Beirut Lebanon.

Kocha huyo hadi umauti ulipomfikia, alikuwa akiinoa Nejmeh ya Lebanon aliyojiunga nayo Februari 9, 2026.

Taarifa ya Nejmeh imethibitisha kifo cha kocha huyo huku ikimsifu kwa weledi wake kwa kipindi chote alichoinoa timu yao.

“Sisi ni wa Mungu na kwake tutarejea. Kwa huzuni na masikitiko makubwa klabu yetu inamlilia Kocha wetu wa kikosi cha kwanza, Engin Firat aliyetangulia kufuatia shambulio la ghafla la moyo katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul akiwa njiani kuelekea Adana, saa chache baada ya kuondoka Beirut kwenda nchini mwake.

“Katika kipindi alichofanya kazi na klabu, marehemu alitambulika kwa weledi wa kujitolea na maadili ya hali ya juu na ameacha muonekano mzuri kwa timu na wanafamilia wa Nejmeh,” imesema taarifa ya klabu yake.

Firat aliinoa Harambee Stars kwa muda wa miaka mitatu kuanzia 2021 hadi 2024.

Mbali na Kenya na Nejmeh, Firat pia amewahi kuzinoa Saipa FC, Sepahan, timu ya taifa ya Iran na timu ya taifa ya Moldova.