Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barcelona yaanza kujipanga kwa Luis Diaz

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Barca inahitaji sana saini ya Diaz ambaye pia ndoto yake ni kuichezea timu hiyo lakini changamoto kubwa ni kiasi cha pesa ambacho Liverpool inakihitaji ili kumuuza, hivyo wanataka kujaribu kufanya mabadilishano.

BARCELONA inafikiria kufanya mabadilishano ya wachezaji na Liverpool na imepanga iwape beki wa kati wa Uruguay, Ronald Araujo, mwenye umri wa miaka 26, ili kumpata winga wa majogoo hao na timu ya taifa ya  Colombia, Luis Diaz, 28, dirisha lijalo.

Barca inahitaji sana saini ya Diaz ambaye pia ndoto yake ni kuichezea timu hiyo lakini changamoto kubwa ni kiasi cha pesa ambacho Liverpool inakihitaji ili kumuuza, hivyo wanataka kujaribu kufanya mabadilishano.

Diaz ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, msimu huu amecheza mechi 43 za michuano yote na kufunga mabao 13.

Kwa sasa vinara hawa wa La Liga wanakutana hali ngumu ya kiuchumi, hivyo itakuwa ngumu kufanya usajili kwa kutoa ada ya uhamisho badala yake watajikita katika kufanya mabadilishano.


Florian Wirtz

MANCHESTER City imezidisha juhudi katika mpango wao wa kutaka kumsajili kiungo wa Bayer Leverkusen na timu ya taifa ya Ujerumani, Florian Wirtz, mwenye umri wa miaka 21, ambaye inamwangalia kama mbadala wa kiungo wao wa kimataifa wa Ubelgiji, Kevin de Bruyne, 33, anayetarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu. Man City ipo tayari kulipa Pauni 100 milioni ili kufanikisha mchakato huo dirisha la majira ya kiangazi litakapofunguliwa.


Jean-Philippe Mateta

MANCHESTER United, Nottingham Forest, Juventus na Bayern Munich zinataka kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace na timu ya taifa ya Ufaransa, Jean-Philippe Mateta, 27, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Vigogo hawa wamevutiwa sana na Mateta kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu na amecheza mechi 36 za michuano yote na kufunga mabao 16.


Noni Madueke

ASTON Villa imepata matumini ya makubwa ya kumsajili winga wa Chelsea, Noni Madueke, 23, baada ya timu hiyo kuwa tayari kumwachia. Madueke anaripotiwa kuwasilisha barua ya kuomba kuuzwa au kutolewa kwa mkopo katika dirisha lijalo ili kutua timu itakayompa nafasi kubwa zaidi ya kucheza baada ya kutoipata akiwa na matajiri hao wa Jiji la London.


Viktor Gyokeres

WAKALA wa mshambuliaji wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres atakuwa katika mechi ya Ligi ya Mabingwa ya Arsenal dhidi ya Real Madrid, huku uvumi ukizidi kusambaa straika huyo wa kimataifa wa Sweden,26, anaweza kutua Arsenal mwisho wa msimu. Inaelezwa wakala huyo ambaye anamsimamia beki wa Madrid, Antonio Rudiger atakuwa uwanjani kumtazama beki huyo na kufanya mazungumzo na Arsenal.


Lamine Yamal

LIVERPOOL na Manchester City zipo macho kodo kuangalia ikiwa zinaweza kumpata mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Lamine Yamal ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu ujao. Hata hivyo, staa huyu mwenye umri wa miaka 17, hana mpango wa kuondoka katika kikosi hicho na anatarajiwa kusaini mkataba mpya hivi karibuni.


Morgan Rogers

KOCHA wa Manchester City ni shabiki mkubwa wa winga wa Aston Villa, Morgan Rogers,ambaye amewasilisha jina lake kwa vigogo wa timu na kutaka asajiliwe dirisha la majira ya kiangazi. Rogers mwenye umri wa miaka 22, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030, msimu huu amecheza mechi 44 za michuano yote na kufunga mabao 13.


Enzo Barrenechea

ASTON Villa ipo tayari kumuuza kiungo wao raia wa Argentina, Enzo Barrenechea, 23, kwenda Valencia na kwa sasa anacheza kwa mkopo katika timu hiyo. Valencia imewasilisha ofa ya kutaka kumsajili fundi huyu baada ya kuvutiwa na kiwango bora alichoonyesha tangu ajiunge nao kwa mkopo msimu huu.