Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Brazil yarudi kwa Ancelotti

BRAZIL Pict

Muktasari:

  • Mazungumzo hayo yameanza tena upya kufuatia kichapo cha aibu cha 4-1 kutoka kwa mahasimu wa jadi, Argentina katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia, usiku wa Jumanne.

SAO PAULO, BRAZIL: SHIRIKISHO la Soka la Brazil limerudi tena mezani kuzungumza na wawakilishi wa kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti kwa ajili ya kumtaka akawe kocha wao mkuu kuelekea Kombe la Dunia la 2026, ripoti inaeleza.

Mazungumzo hayo yameanza tena upya kufuatia kichapo cha aibu cha 4-1 kutoka kwa mahasimu wa jadi, Argentina katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia, usiku wa Jumanne.

 Matokeo hayo yaliwaacha Brazil katika nafasi ya nne kwenye msimamo ambao timu sita za juu zinafuzu moja kwa moja ushiriki wa mashindano hayo yatakayofanyika Marekani, Mexico na Canada.

Brazil walianza kumfuatilia kocha huyu mwenye umri wa miaka 65 mwaka 2023 ambapo walikuwa tayari kumfanya kuwa kocha wao wa kwanza wa kigeni katika historia ya taifa hilo, lakini ilishindikana.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Athletic, tangu wakati huo shirikisho la nchi hiyo limekuwa katika mawasiliano na Muitaliano huyo huku shinikizo likiongezeka kwa kocha anayeshikilia wadhifa, Dorival Junior kutokana na matokeo yao ya sasa.

Rais wa Shirikisho la Soka la Brazil, Ednaldo Rodrigues, ambaye alichaguliwa tena wiki hii bila kupingwa, aliwahi kusema Ancelotti alikuwa ajiunge na timu hiyo mwaka 2024 mara baada ya mkataba wake na Madrid kumalizika muda mfupi  kabla ya michuano ya Copa America iliyofanyika Marekani lakini ilishindikana.

Brazil ilimteua Fernando Diniz kushughulikia timu kwa muda kabla ya kumwajiri  kocha mkuu wa Fluminense, Junior kuwa kocha mkuu.

Lejendi wa timu ya taifa ya Brazil, Ronaldo alifichua kuwa Madrid walikuwa karibu kumfuta kazi Ancelotti, jambo ambalo ndio lililkuwa linawapa matumaini makubwa kwamba wangempata lakini ilishindikana.