Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dah! Chiesa awekwa sokoni Liverpool kina Salah wakibaki

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Chiesa amekuwa na wakati mbaya tangu atue Liverpool mwaka jana na anadaiwa kuomba kuondoka ili kupata nafasi ya kucheza sehemu nyingine.

WAKATI Liverpool imefanikiwa kuwabakisha mastaa wake wawili Mohamed Salah na Virgil van Dijk, klabu hiyo inahitaji Pauni 17 milioni katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kumuuza mshambuliaji wao raia wa Italia, Federico Chiesa, 27, ambaye anawindwa na AC Milan na baadhi ya timu za England.

Chiesa amekuwa na wakati mbaya tangu atue Liverpool mwaka jana na anadaiwa kuomba kuondoka ili kupata nafasi ya kucheza sehemu nyingine.

Moja kati ya vitu ambavyo vimechangia sana Chiesa kutoonyesha kiwango kilichotarajiwa ni hali ya majeraha ya mara kwa mara ambayo amekuwa nayo tangu ajiunge na majogoo hao.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

Msimu huu amecheza mechi 12 za michuano yote na kufunga mabao mawili.


Dean Huijsen

CHELSEA inakumbana na upinzani kutoka kwa timu nyingine za Ligi Kuu England katika harakati zao za kuiwania saini ya beki kisiki wa Bournemouth, Dean Huijsen ambaye inahitaji kumsajili katika dirisha lijalo la makora ya kiangazi.

Dean mwenye umri wa miaka 19, anawindwa na timu nyingi kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu.


Jesus Rodriguez

REAL Betis imeweka wazi kwamba timu yoyote inayohitaji huduma ya winga wao Jesus Rodriguez itatakiwa kutoa Pauni 42 milioni kama ada ya uhamisho ambayo imewekwa katika kipengele kimojawapo cha mkataba wake.

Mkataba wa sasa wa Rodriguez unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.

Betis imekuwa na msimu mzuri baada ya kusajili wakali kadhaa wakiwamo wa mkopo kama Antony.


Luka Modric

REAL Madrid wako tayari kumruhusu kiungo wao mkongwe Luka Modric, 39, kuondoka katika dirisha la majira ya kiangazi ambapo mkataba wake utakuwa unamalizika.

Awali, ilielezwa kwamba Madrid wanataka kumsainisha mkataba mpya lakini sasa mambo yanaonekana kubadilika. Msimu huu amecheza mechi 48 za michuano yote na kufunga mabao manne. Mwaka atakuwa na miaka 40.


Arda Guler

ARSENAL wamepanga kutoa ofa ya Pauni 35 milioni kwenda Real Madrid ili kuipata huduma ya winga wa wababe hao na timu ya taifa ya Uturuki, Arda Guler, 20, katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu.

Guler amekuwa akihusishwa kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Madrid, ambacho kina ushindani mkubwa wa kugombea namba.


Florian Wirtz

MKURUGENZI mkuu wa Bayer Leverkusen, Fernando Carro, ana matumaini makubwa kwamba kiungo wao mshambuliaji na timu ya taifa ya Ujerumani, Florian Wirtz mwenye umri wa miaka 21, ataendelea kuwepo kwa msimu ujao pamoja na kocha wao Xabi Alonso.

Wirtz ni mmoja kati ya viungo wanaowindwa na Manchester City tangu Januari mwaka huu.


Ederson

MANCHESTER United inatarajia kuwasilisha ofa rasmi kwenda Atalanta kwa ajili ya kumsajili kiungo wa timu hiyo na timu ya taifa ya Brazil, Ederson, mwenye umri wa miaka 25, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Atalanta ipo tayari kumuuza fundi huyu lakini kwa kiasi cha pesa ambacho hakitopungua Pauni 52 milioni.

Tangu kuanza kwa msimu huu Ederson amecheza mechi 42 za michuano yote na kufunga mabao manne.


Nicolo Barella

LIVERPOOL inajiandaa kutuma ofa kwenda Inter Milan kwa ajili ya kumsajili kiungo wa timu hiyo na Italia Nicolo Barella, 28, katika dirisha lijalo.

Barella ni mmoja kati ya mastaa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Inter na msimu huu amecheza mechi 42 za michuano yote na kufunga mabao matatu, mkataba wake unamalizika mwaka 2029.