Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ekitike azidi kuwa lulu Ujerumani

LULU Pict

Muktasari:

  • Saini ya nyota huyu wa kimataifa wa Ufaransa ambaye ameonyesha kiwango bora katika Bundesliga msimu huu na amefunga mabao 19 katika mechi 38 za mashindano mbalimbali, inahitajika na Arsenl, Liverpool na Man United.

FRANFURT, UJERUMANI: MSHAMBULIAJI wa Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike ameziweka njiapanda timu kubwa England zinazohitaji saini yake dirisha ljalo.

Saini ya nyota huyu wa kimataifa wa Ufaransa ambaye ameonyesha kiwango bora katika Bundesliga msimu huu na amefunga mabao 19 katika mechi 38 za mashindano mbalimbali, inahitajika na Arsenl, Liverpool na Man United.

Ekitike ameweka wazi moja kati ya ndoto zake tangu akiwa mtoto mdogo ni kucheza katika ligi ya EPL na sasa inaonekana kwenda kutumia.

Mshambuliaji huyu alijiunga na Frankfurt kwa mkopo akitokea PSG Januari 2024 kabla ya upande wa timu hiyo kuvutiwa naye na kumsanisha mkataba wa kudumu kwa kutoa Pauni 13.2 milioni dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana.

Ekitike ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya Ufaransa ya chini ya miaka 21 alionyesha uwezo wake wakati wa mapumziko ya kimataifa, alipofunga hat-trick dhidi ya timu ya chini ya miaka 21 ya England iliyokuwa chini ya Lee Carsley.

Hata hivyo, licha uwepo wa Arsenal na Liverpool moja kati ya timu ambazo Ekitike amesema alipokuwa mtoto alipenda kuzichezea ni Manchester United.

Ekitike bado ana miaka minne katika mkataba wake ambao unamfanya apate takribani Pauni 50,000 kwa wiki kiasi ambacho anaweza kulipwa mara mbili au mara tatu akitua England.

Hivi karibuni, Mario Goetze alizungumzia mchezaji huyu akisema:"Ana ujuzi ambao wachezaji wachache wanao. Ana ufanisi wa kukokota mpira, kumalizia, na kasi. Yeye ni thamani ya ziada kwa timu."

Man United chini ya Ruben Amorim wanatarajiwa kusajili mshambuliaji mwisho wa msimu kutokana na matatizo yao katika eneo hilo.

Joshua Zirkzee hajaonyesha kilichotarajiwa tangu atue sawa na ilivyokuwa kwa Rasmus Hojlund, kwa upande wa Arsenal yenyewe pia ina mapungufu katika eneo hilo pia kwa upande wa Liverpool inatafuta mbadala wa Mohamed Salah ambaye anatarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu.