Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gundogan ataja tatizo kushuka kwa Man City

Muktasari:

  • Licha ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England mara nne mfululizo na mara sita katika misimu saba iliyopita, kikosi hicho cha Pep Guardiola kimekuwa na wakati mgumu kuendeleza kiwango bora msimu huu.

MANCHESTER, ENGLAND: KIUNGO wa Manchester City, Ilkay Gundogan amesema kati ya vitu vilivyochangia kushuka kwa kiwango cha timu ni baadhi ya wachezaji kupoteza hamu ya kutawala na kushinda mechi kama ilivyokuwa zamani.

Licha ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England mara nne mfululizo na mara sita katika misimu saba iliyopita, kikosi hicho cha Pep Guardiola kimekuwa na wakati mgumu kuendeleza kiwango bora msimu huu.

Matokeo mabaya kiliyopata kati ya Novemba na Desemba, mwaka jana yalisababisha kishuke hadi nafasi ya sita katika msimamo.

Kwa sasa kimebakisha mechi saba na kila mchezo umekuwa wa muhimu kwao kwani kinataka kumaliza katika nafasi tano za juu zitakazokihakikishia kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Gundogan, aliyekuwa nahodha wa Man wa City wakati ilipotwaa mataji matatu msimu uliopita, amedokeza kukosa kasi, matamanio na shauku ni sababu iliyowafanya kuwa katika nafasi waliyopo sasa.

Katika mahojiano na ESPN, Gundogan alisema matatizo ya Man City hayajahusiana tu na mbinu au majeraha, bali pia ni ya kisaikolojia. Anaamini kwamba kuangalia masuala ya mifumo kama ndio sababu ya anguko ni makosa na badala yake kuna mambo madogo ambayo hayasemwi yanachangia sana wao kuwa katika hali hiyo.

“Ninaona  kama kwenye mechi nyingi, tulitilia mkazo sana mbinu za mchezo na hatukuweka maanani vitu kama msukumo wa kufanya jambo, hamu na kujitoa kwa nguvu zote ambavyo ni sehemu ya mchezo na huchangia sana timu kupata ushindi.”