Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kesi ya Man City yapigwa kalenda

MAN CITY Pict

Muktasari:

  • Ligi Kuu Englanda imeishatuhumu Man City kwa mashitaka 130, wakidaiwa kuvunja kanuni za usawa wa kifedha  kati ya mwaka 2009 na 2018, pia inatuhumiwa kushindwa  kutoa ushirikiano na mamlaka katika masuala ya uchunguzi.

MANCHESTER, ENGLAND: LICHA ya ripoti kudai kwamba kesi yao inaweza kutolewa hukumu kabla ya dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu, sasa Manchester City itatakiwa kusubiri kwa muda mrefu zaidi kabla ya kujua hatma yao juu ya mashtaka 130 yanayowakabili.

Ligi Kuu Englanda imeishatuhumu Man City kwa mashitaka 130, wakidaiwa kuvunja kanuni za usawa wa kifedha  kati ya mwaka 2009 na 2018, pia inatuhumiwa kushindwa  kutoa ushirikiano na mamlaka katika masuala ya uchunguzi.

Hata hivyo, matajiri hao wa Jiji la Manchester wamekana vikali mashitaka yote na wamesisitiza kuwa wanahitaji ushahidi zaidi juu ya mashtaka hayo.

Kocha wa Man City, Pep Guardiola, Februari mwaka huu alisema anatarajia kukumu hiyo kutoka ndani ya muda mfupi.

"Ni ndani ya mwezi mmoja labda naona hukumu itatoka, baada ya hapo, nitatoa maoni yangu."

Hata hivyo, The Telegraph sasa inaripoti kwamba kuna uwezekano kuwa kesi hiyo ikachukua muda mrefu zaidi kabla ya hukumu kufikiwa.

 Ripoti inasema kwamba kulikuwa na matumaini ya kutolewa kwa uamuzi mapema, lakini idadi ya mashitaka, kiasi cha ushahidi, na changamoto zinazohusiana na kesi hiyo vimesababisha ucheleweshaji, hivyo, kuna uwezekano kwamba msimu wa 2025/26 utaanza bila ya hukumu ya kesi hiyo kutolewa.

Mshambuliaji nyota Erling Haaland alisaini mkataba mpya wa miaka tisa na nusu na City Januari iliyopita na alipoulizwa kwa nini aliamua kujitolea kwa mkataba wa muda mrefu na klabu licha ya kesi kuendelea kuunguruma alisisitiza kuwa hajali.