Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kevin De Bruyne kambi kokote

KBD Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 alikuwa akizungumza na mwandishi wa habari wa Norway, Jan Aage Fjortoft, kuhusu mustakabali wake na alipoulizwa akathibitisha kwamba bado angetamani kucheza soka la kiushindani.

MANCHESTER, ENGLAND: KIUNGO wa Manchester City, Kevin De Bruyne ambaye anatarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu, amesema yupo tayari kupokea ofa ya kucheza kokote ifikapo dirisha lijalo la majira ya kiangazi hata ikiwa ni timu ya ndani ya England.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 alikuwa akizungumza na mwandishi wa habari wa Norway, Jan Aage Fjortoft, kuhusu mustakabali wake na alipoulizwa akathibitisha kwamba bado angetamani kucheza soka la kiushindani.

"Sijui nini kitatokea msimu ujao. Kama timu zitakuja na kunishawishi kwamba zina ofa nzuri na mpango mzuri, nitazingatia, najua kwa sasa mimi sio kijana tena, lakini bado naamini ninaweza kucheza katika soka la kushindani, sijui ni timu gani itavutiwa nami, lakini nitakuwa tayari kusikiliza ofa za timu zitakazokuja mezani. Napenda soka, napenda kucheza soka, na kama ofa nzuri itatokea na familia yangu itakubaliana nayo, basi tutaweza kufanya uamuzi," alisema De Bruyne.

Staa huyu alipoulizwa kama atabakia England alisema:" "Sijui kwakweli. Uamuzi wa kuondoka hauna muda mrefu tangu utolewe, siwezi kuamua ndani ya wiki moja, hadi sasa bado sijakutana na familia yangu tangu uamuzi huo utolewe, inabidi nizungumze nao kisha nitaangalia ni timu gani zitakazohitaji huduma yangu. Hivyo basi kwa sasa sijui."

Mapema wiki hii iliyopita, ilitangazwa kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ataondoka Man City baada ya kuhudumu kwa misimu kumi.

Anaondoka akiwa ameshinda medali sita za ubingwa wa Ligi Kuu England, moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, na tuzo mbili za Mchezaji Bora wa mwaka wa England.