Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Isak, mastraika kibao wawindwa

Isak Pict

Muktasari:

  • Isak, 25, amejipambanua kama mmoja wa Namba 9 hatari kabisa kwenye Ligi Kuu England tangu alipojiunga na Newcastle mwaka 2022 na kwamba amezidiwa na Mohamed Salah na Erling Haaland kwenye mabao ya kufunga msimu huu.

NEWCASTLE, ENGLAND: NEWCASTLE United imeweka ubaoni orodha ya mastraika matata ili kujiandaa endapo kama Alexander Isak ataamua kuondoka, licha ya kwamba hawana mpango wa kumuuza fowadi huyo wa kimataifa wa Sweden.

Isak, 25, amejipambanua kama mmoja wa Namba 9 hatari kabisa kwenye Ligi Kuu England tangu alipojiunga na Newcastle mwaka 2022 na kwamba amezidiwa na Mohamed Salah na Erling Haaland kwenye mabao ya kufunga msimu huu.

Arsenal imekuwa ikimfukuzia straika huyo wa zamani wa Real Sociedad kwa miezi sasa ikihitaji mtu wa maana akaongoze safu yao ya ushambuliaji. Liverpool nayo imekuwa ikimsaka mchezaji huyo ili kwenda kuchukua mikoba ya Darwin Nunez, ambaye anaweza kufunguliwa mlango aondoke Anfield.

Mpango wa Newcastle upo palepale, kwamba hawana mpango wa kumuuza Isak na ipo tayari kuanzisha mazungumzo ya mkataba mpya itakapofika mwisho wa msimu.

Lakini, hilo haliwazuii wao kuweka kwenye mipango yao juu ya mastraika wengine inaotaka kuwasajili, ikiweka ubaoni majina ya wakali kibao akiwamo Benjamin Sesko.

Straika huyo wa RB Leipzig anaripotiwa pia kuwa kwenye rada za Arsenal, ambao wataingia sokoni kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi kunasa huduma ya straika wa kiwango cha dunia baada ya kushindwa Januari.

Sambamba na Sesko, Newcastle United pia imekuwa ikivutiwa na Jonathan David na Liam Delap, ambaye amekuwa na kiwango bora kabisa kwenye kikosi cha Ipswich Town, licha ya timu yake kufanya vibaya Ligi Kuu England.

Delap ni mchezaji mwingine ambaye atasumbua timu kwenye dirisha lijalo la uhamisho baada ya kufunga mabao 10 kwenye Ligi Kuu England msimu huu. Manchester United na Chelsea nazo zimekuwa zikimfuatilia mchezaji huyo, ambaye aliwahi kukipiga Manchester City kabla ya kutua Suffolk.