Man City ikishinda kesi, klabu za EPL imekula kwao

Muktasari:
- Wapinzani hao wa Man City huenda wakalazimika kulipa Pauni 5 milioni kila mmoja kama fidia ya kesi hiyo na ni endapo City ikishinda kesi hiyo iliyochukua muda mrefu tangu Februari 2023 ilipoanza kusikilizwa na yenye mashitaka 130.
MANCHESTER, ENGLAND: KESI ya kisheria kati ya Manchester City na mamlaka zinazosimamia Ligi Kuu England huenda ikaibua mapya na kuzigharibu klabu zinazoshiriki Ligi Kuu England kwa kutakiwa kuilipa fidia miamba hiyo ya Etihad.
Wapinzani hao wa Man City huenda wakalazimika kulipa Pauni 5 milioni kila mmoja kama fidia ya kesi hiyo na ni endapo City ikishinda kesi hiyo iliyochukua muda mrefu tangu Februari 2023 ilipoanza kusikilizwa na yenye mashitaka 130.
Inaaminika gharama za kisheria kwa pande zote, yaani Ligi Kuu na Manchester City, zinaweza kufikia zaidi ya Pauni 100 milioni hadi kufikia siku yamwisho ya hukumu.
inatoka uk 20
Hata hivyo, ikiwa Man City itajitetea na kushinda kuna uwezekano mkubwa wakadai kurejeshewa gharama zao zote, zitakazolipwa na timu nyingine 19 zilizopo katika ligi.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, gharama kama hizo hutolewa kutoka kwenye mapato ya kila mwaka ya mikataba ya haki za matangazo na mapato mengine.
Hili litakuwa pigo kubwa la kiuchumi kwa timu nyingi ambazo zinahaha kuhakikisha zinaingiza mapato na kuendana na sheria ya matumizi ya fedha.
Kwa mujibu wa ripoti, hadi sasa kuna mashtaka 130 dhidi ya Man City, yakiwemo madai ya kuficha mapato ya udhamini, kumlipa kocha wao wa zamani, Roberto Mancini nje ya mkataba wake, kutotoa maelezo kamili kuhusu mishahara ya wachezaji na kushindwa kushirikiana ipasavyo na mamlaka za uchunguzi kwa nyakati mbili tofauti.
Adhabu kali zaidi kwa ukiukwaji huu inaweza kuwa ni kushushwa katika ligi lakini hadi sasa hakuna ishara ya hukumu kutolewa hivi karibuni, gazeti la The Times limeripoti kesi hii huenda ikaendelea hadi mwaka 2026.