Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki Spurs waandamana

Muktasari:

  • Spurs wamekuwa wakipitia kipindi kigumu tangu kuanza kwa msimu huu na walipokea kichapo chao cha 16 katika ligi baada ya kufungwa na Chelsea Alhamisi iliyopita.

LONDON, ENGLAND: MASHABIKI wa Tottenham waliandamana katika mitaa mbalimbali na nje ya uwanja wao wa Tottenham Hotspur Stadium wakimtaka mwenyekiti wao Daniel Levy kuachana na timu hiyo.

Spurs wamekuwa wakipitia kipindi kigumu tangu kuanza kwa msimu huu na walipokea kichapo chao cha 16 katika ligi baada ya kufungwa na Chelsea Alhamisi iliyopita.

Mashabiki walionyesha hisia zao wazi dhidi ya wachezaji na kocha Ange Postecoglou kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mara baada ya mchezo huo kumalizika.

Mbali ya hasira kwa kocha na  wachezaji, mashabiki hao pia wamehamia kwa Levy ambaye wanaamini ndio anarudisha maendeleo ya timu hiyo nyuma kwa sababu hawekezi inavyotakiwa, pia uongozi wake ni mbaya.

Mashabiki hao walionekana wakiwa na mabango yanayotaka Levy aondoke kwenye klabu, huku wakitoa wito wa mabadiliko.

Mbali ya mabango, wengine walikuwa wakiimba huku wakishangilia “Tunataka Levy aondoke!” na “Daniel Levy, ondoka katika klabu yetu!”

Mashabiki pia walionyesha hasira zao kwenye mtandao wa X (zamani Twitter) ambapo mmoja aliandika: “Yatosha, hali ya klabu hii ni aibu kabisa. Tunahitaji mabadiliko kamili, na kitu cha kwanza kubadilika ni umiliki na wale wanaofanya uamuzi.”

Mwingine aliandika: “Najivunia sana kwa wote waliohusika katika maandamano. Klabu yetu inahitaji mabadiliko.”

Levy mara nyingi anashutumiwa kwa kutojali mafanikio ya soka uwanjani.

Lakini yeye amekataa malalamiko hayo, akisema: “Tangu tumefungua uwanja wetu mpya Aprili 2019, tumefanya uwekezaji wa zaidi ya Pauni 700 milioni kununua wachezaji.”

“Usajili bado ni kipaumbele chetu lakini lazima tuhakikishe tunafanya manunuzi ya busara yaliyo ndani ya uwezo wetu wa kifedha.”

“Mara nyingi nasoma wito wa sisi kutumia zaidi, na hiyo najua ni kwa sababu tumeorodheshwa kama klabu ya tisa tajiri zaidi duniani.”

“Hata hivyo, uchambuzi wa karibu wa takwimu za kifedha za leo unaonyesha kuwa matumizi hayo lazima yawe endelevu kwa muda mrefu na yawe yanatoka ndani ya mapato yetu ya uendeshaji.”