Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mechi ya kisasi Ulaya

Kisasi Pict
Kisasi Pict

Muktasari:

  • Huenda mashabiki wa Liverpool bado hawajaisamehe Madrid baada ya kufungwa kwenye fainali ya msimu wa 2017/18 walipopoteza kwa mabao 3-1.

LIVERPOOL, ENGLAND: Ligi ya Mabingwa Ulaya inarudi tena usiku huu na mechi kali inayosubiriwa kwa hamu ni katika dimba la Anfield, kuanzia saa 5:00 usiku na Liverpool itaikaribisha Real Madrid.

Huenda mashabiki wa Liverpool bado hawajaisamehe Madrid baada ya kufungwa kwenye fainali ya msimu wa 2017/18 walipopoteza kwa mabao 3-1.

Madrid pia iliwaachia  maumivu mashabiki hao baada ya Sergio Ramos kumchezea rafu, Mohemed Salah na kumvunja bega.

Kisasi hicho hadi sasa hakijalipwa kwani baada ya mchezo huo, timu hizi zimekutana mara tano na Liverpool imepoteza nne na kutoa sare moja tu.

Vilevile katika mechi hizo tano, moja pia ilikuwa ni ya fainali msimu wa 2021/22 ambao ulimalizika kwa Liverpool kupoteza kwa bao 1-0.

Katika fainali ya mwaka 2017/18, moja kati ya mambo yaliyowauma zaidi mashabiki wa Liverpool ilikuwa ni makosa makubwa yaliyofanywa na kipa wao Loris Karius.

Matukio yanaonyesha hii huenda ikawa mechi ya kisasi kwa Liverpool kurudisha yale iliyofanyiwa kwa kushinda mechi hii.

Vile vile Liverpool itakuwa inahitaji kushinda kwa mara ya kwanza mbele ya Madrid tangu msimu wa 2008/09 na ilishinda mchezo wa hatua ya 16 bora na ilishinda mabao 4-0.

Huenda hii ikawa ni nafasi kwa Liverpool kwani inakutana na Madrid ambayo msimu huu imekuwa na panda shuka kadhaa.

Kwanza inaelezwa kuna migogoro baina ya mastaa na hata benchi la ufundi inadaiwa Carlo Ancelotti haelewani na idara ya matibabu hususani kocha wa viungo.

Pia timu hiyo ambayo ndio bingwa mtetezi wa michuano hii, itawakosa wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza, Vinicius Jr, Rodrygo, Eder Militao, Aurelien Tchouameni, David Alaba, Dani Carvajal.

Kijumla timu hizi zimekutana mara 11 Ligi ya Mabingwa na Madrid imeshinda saba, sare moja na Liverpool ikashinda tatu.

Kwa sasa Liverpool ndio inaongoza katika msimamo wa Ligi ya Mabingwa ikiwa imecheza mechi nne na kushinda zote wakati Madrid ikiwa nafasi ya baada ya kushinda mechi mbili na kupoteza mbili kati ya nne.

Mbali ya mchezo huu, leo pia kutakuwa na mechi nyingine sita za muchuano hii na mechi nyingine inayoonekana kuwa itavutia zaidi ni kati ya  Aston Villa na Juventus.

Ikiwa Villa itafanikiwa kushinda mchezo huu inaweza kupanda hadi nafasi nne za juu kwa kufikisha pointi 12 wakati Juventus ikishinda itapanda hadi nafasi nane za juu.

Mechi nyingine inayoonekana itatazamwa na watu wengi ni kati ya Dinamo Zagreb na Borussia Dortmund na ikiwa Dortmund itashinda inaweza kupanda juu zaidi na hata kuishusha Liverpool ikiwa itapoteza mbele ya Madrid.