Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mshauri wa Trump ataka Iran iondolewe Kombe la Dunia 2026

MSHAURI Pict

Muktasari:

  • Iran ilifuzu kama moja ya timu nane kutoka Asia, wakati Italia ilishindwa kupata nafasi kati ya timu 16 za Ulaya ikiwa ni kwa mara ya tatu mfululizo.

WASHINGTON, MAREKANI: MSHAURI wa ngazi za juu wa Rais wa Marekani,  Donald Trump ameripotiwa kuiomba FIFA kuiondoa timu ya taifa ya Iran katika mashindano ya  Kombe la Dunia na kuipa nafasi hiyo Italia  kutokana na mvutano unaoendelea kati ya Iran na Marekani.

Mzozo huo uliochochewa na mashambulizi ya pamoja ya Marekani na Israel dhidi ya Iran Februari mwaka huu kiasi cha kuanzisha vita, umeweka mashaka juu ya ushiriki wa Iran katika michuano hiyo ya inayotarajiwa kuanza Juni 11 huko Marekani, Canada na Mexico.

Kulikuwa na hofu kuwa shirikisho la soka la Iran lingeweza kususia mashindano hayo, lakini mpango huo kwa sasa unaonekana kuwa haupo baada ya kikao cha ana kwa ana kati ya Rais wa FIFA Gianni Infantino na wawakilishi wa Iran.

Katika kikao hicho, Infantino aliahidi kutoa msaada wa maandalizi kwa timu hiyo, hasa ikizingatiwa ligi ya ndani ya Iran imesimamishwa kutokana na vita.

Kwa mujibu wa Financial Times, mjumbe maalum wa Marekani Paolo Zampolli amependekeza kwa Trump na Infantino kuwa Italia ichukue nafasi ya Iran.

Zampolli, ambaye alizaliwa Milan, anadaiwa kusema historia ya Italia kama mabingwa wa dunia mara nne inawapa sifa ya kustahili nafasi hiyo, licha ya kushindwa kufuzu.

Inadaiwa pia pendekezo hilo lina uhusiano wa juhudi za kurekebisha mahusiano kati ya Trump na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni baada ya kutofautiana kuhusu kauli za Trump dhidi ya Pope Leo XIV.

Hata hivyo, shirikisho la soka la Iran limesisitiza wana asilimia kubwa wa kushiriki mashindano hayo.

Iran ilifuzu kama moja ya timu nane kutoka Asia, wakati Italia ilishindwa kupata nafasi kati ya timu 16 za Ulaya ikiwa ni kwa mara ya tatu mfululizo.