Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwisho kesho, FIFA kupokea orodha ya wachezaji Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Jumla ya wachezaji 1,248 wanategemewa kushiriki fainali hizo zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico kuanzia Juni 11 hadi Julai 19, mwaka huu.

Muda wa siku tisa tu ndio umebakia kabla ya kuanza kwa fainali hozo zitakazofanyika kuanzia Juni 11 hadi Julai 19 mwaka huu.

Jumla ya wachezaji 1,248 wanategemewa kushiriki fainali hizo zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico kuanzia Juni 11 hadi Julai 19, mwaka huu.

Kila timu ina nafasi ya kutumia wachezaji 26 na kati ya hao, watatu ni lazima wake makipa.

Vikosi hivyo ambavyo kesho ni siku ya mwisho kutambulishwa, ni lazima vitokane na orodha ya awali vya wachezaji 33 hadi 55 ambavyo mwisho wa kuwasilishwa ulikuwa ni Mei 11, 2026.

Ingawa orodha hiyo ni ya mwisho, Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) huruhusu mabadiliko iwapo kunatokea dharura maalum kwa mujibu wa kanuni.

Ili timu iruhusiwe kumuingiza mchezaji na kumtoa mwingine kikosini mara baada ya kuwasilisha majina leo, inatakiwa ifanye hivyo kwa mchezaji ambaye amepata ugonjwa au jeraha kubwa ambalo litamfanya asiwe na uwezo wa kucheza mashindano hayo hadi yatakapomalizika.

Hata hivyo, hilo linapaswa kufanyika hadi saa 24 kabla ya mechi ya kwanza ya timu husika.

Hii ni mara ya pili kwa Marekani kuandaa fainali hizo, ya kwanza ikiwa ni 1994 na Mexico wanaandaa fainali hizo kwa mara ya tatu baada ya kufanya hivyo miaka ya 1970 na 1986 huku Canada ikiwa ndio inaandaa kwa mara ya kwanza.

Bosnia & Herzegovina ndio timu ya kwanza kuwasilisha orodha ya nyota wake ambao itawatumia katika Fainali za Kombe la Dunia 2026.