Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi aing'oa Mamelodi, aifuata Orlando fainali

NABI Pict

Muktasari:

  • Kaizer  inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga na FA Rabat ya Morocco, Nasredine Nabi imelazimika kutoka nyuma kutengeneza ushindi huo, kwani ilitangulia kuruhusu bao dakika 45+5 lililowekwa kimiani na kiungo Teboho Mokoena kwa shambulizi la adhabu ndogo.

KAIZER Chiefs, imesitisha unyonge mbele ya Mamelodi Sundown baada ya kuichapa kwa mabao 2-1 katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Nedbank na kutinga fainali na sasa inatarajiwa kuvaana na wapinzani wao wa jadi, Orlando Pirates iliyowatupa nje Marumo Galants.

Kaizer  inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga na FA Rabat ya Morocco, Nasredine Nabi imelazimika kutoka nyuma kutengeneza ushindi huo, kwani ilitangulia kuruhusu bao dakika 45+5 lililowekwa kimiani na kiungo Teboho Mokoena kwa shambulizi la adhabu ndogo.

Hata hivyo, Kaizer ikionyesha utulivu wa mipango uwanjani ikafanikiwa kusawazisha bao hilo kipindi cha pili katika dakika ya 57 kupitia mshambuliaji Wandile Duba, aliyeunasa mpira kutoka kwa mabeki wa kati wa Mamelodi wakiwa wanagongeana pasi eneo lao la ulinzi.

Mabadiliko yaliyofanywa na Nabi katika dakika ya 80 ya kumtoa Duba mfungaji wa bao la kusawazisha kisha kumuingiza Ashley Du Preez, yakaibeba Kaizer kwa kuandika bao la pili na la ushindi lililofungwa na mtoa benchi huyo dakika ya 89 na kuwazima wenyeji kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Loftus Versfeld.

Kabla ya mchezo huo, Kaizer Chiefs maarufu kwa jina la Amakhosi haikuwa na matokeo mazuri, ambapo kwenye mechi zake nne za Ligi ikipoteza mbili na kutoa sare mbili, matokeo ambayo yalimuweka Nabi kwenye presha kubwa.

Kaizer sasa inakwenda kukutana na watani wao wa jadi, Orlando Pirates iliyotangulia kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Marumo Gallants kwenye katika mchezo mwingine wa nusu fainali ya kwanza uliopigwa jana kwenye wanja wa Moses Mabhida.

Mechi ya fainali kwa wapinzani hao wa jadi utapigwa Mei 10 ili kupata bingwa wa michuano hiyo ambayo kwa sasa watetezi ni Orlando iliyotwaa msimu uliopita kwa kuwanyoa Mamelodi Sundowns kwa mabao 2-1, huku Kaizer ikiwa ndio vinara wa kutwaa mara nyingi taji hilo ilikibeba mara 13.

Mara ya mwisho kwa Amakhosi kutwaa taji hilo ilikuwa msimu wa 2012-2013 ilipoitambia Super Sport kwa bao 1-0 na mechi hiyo ya Mei 10, itakuwa ni kutaka kuoboresha rekodi ya kulibeba kwa mara ya 14 au kuipa nafasi Orlando kufikisha taji la 11 kwani kwa sasa imelibeba mara 10.