Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais PSG akutana na Mbappe kujadili uhamisho wake

Muktasari:

Mwishoni mwa wiki iliyopita iliripotiwa kwamba Arsenal walitangaza kuweka mezani dau la usajili linalofikia Pauni 125 milioni.

Ufaransa. Mchezaji anayetajwa kuwakosesha usingizi mabosi wa klabu za Real Madrid na Arsenal, Kylian Mbappe anatarajia kukutana na Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi akiwa na Mkurugenzi wa Michezo, Antero Henrique, huku nyota huyo akisindikizwa na baba yake mzazi ili kuzungumzia uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita iliripotiwa kwamba Arsenal walitangaza kuweka mezani dau la usajili linalofikia Pauni 125 milioni.

Hata hivyo mabingwa wa soka barani Ulaya, klabu ya Real Madrid imekuwa ikimfuatilia mchezaji huyo kwa ukaribu.