Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ratcliffe Man United ni sehemu tu ya anavyomiliki, ni tajiri haswa

ATM Pict

Muktasari:

  • Bosi huyo mkubwa ambaye alikuja nchini na kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan na kufanya mazungumzo kuhusu masuala ya utalii, ni mmoja wa watu wanaopenda shughuli hizo licha ya uwekezaji mkubwa aliofanya kwenye michezo.

LONDON, ENGLAND: MOJA ya stori kubwa nchini wiki iliyopita ni ujio wa bilionea mmiliki wa klabu ya Manchester United ya Ligi Kuu England, Jim Ratcliffe.

Bosi huyo mkubwa ambaye alikuja nchini na kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan na kufanya mazungumzo kuhusu masuala ya utalii, ni mmoja wa watu wanaopenda shughuli hizo licha ya uwekezaji mkubwa aliofanya kwenye michezo.

Katika klabu hiyo anamiliki hisa asilimia 25 na ana jukumu la kusimamia masuala yote ya soka ikiwamo usajili na anasubiri kuona itakuaje kwenye usajili wa dirisha kubwa lijalo la majira ya kiangazi kwani timu hiyo kwa sasa inasuasua katika michuano mbalimbali inayoshiriki.

Ratcliffe anamiliki klabu kadhaa za soka na kampuni mbalimbali na zimemfanya kuendelea kuwa tajiri bilionea na hapa ATM inakuletea namna anavyopiga pesa kutokana na uwekezaji wake.

AT 04

ANAPIGAJE PESA

Mwaka 2023, gazeti la The Sunday Times ilifichua Ratcliffe ni tajiri namba 27 duniani na unakadiriwa kufikia Dola 7.4 bilioni, hata hivyo, inakadiriwa utajiri huo unaofikia Dola 16.3 bilioni.

Utajiri huu unatokana na faida kubwa anayoipata kutokana na kampuni yake ya Ineos ambayo kwa mwaka huingiza mapato ya zaidi ya Dola 61 bilioni.

Kampuni hiyo inajihusisha na uzalishaji na uchakataji wa mafuta ya petroli, gesi, kemikali na plastiki.

Ndani yake kuna kampuni ndogo ndogo zisizopungua 22 ambazo zote kwa pamoja zinatoa zaidi ya Dola 5 bilioni kama faida kila mwaka.

Tajiri huyu pia ana kampuni ya utengenezaji wa magari iitwayo The INEOS Grenadier 4X4.

Mwaka 1998, kampuni yake ya Ineos iliweka rekodi ya kuwa moja kati ya kampuni kubwa nne zinazoongoza kwa uchakataji wa mafuta na kemikali duniani, hii ilikuwa ni miaka mitatu tu baada ya kuinunua kwa Pauni 75 milioni mwaka 1995.

Hadi kufikia mwaka 2021, INEOS na kampuni nyingine ndogo zilizo chini yake zilikuwa zimeajiri watu 26,000 kwa ajira rasmi.

Kwa sasa makao makuu ya kampuni yapo kule England na Marekani lakiki viwanda vyake vimesambaa bara zima la Ulaya.

Mbali ya Man United, Ratcliffe anamiliki pia timu nyingine za mpira wa miguu ambao ni FC Lausanne inayoshiriki Ligi Kuu Uswiss na Nice inayocheza Ligi Kuu Ufaransa.

AT 01

MIJENGO

Ana mijengo ya kifahari katika nchi tatu ambazo ni Ufaransa ambako katika kisiwa cha Monaco, pia nyingine ipo Geneva Uswiss karibu na mjengo wa dereva wa zamani wa magari ya mashindano F1,  Michael Schumacher wenye thamani ya Pauni 5 milioni. Pia ana nyumba Nottingham, England.

Nyumba zake za Ufaransa na Uswiss zipo karibu na bahari kwa kuwa tajiri huyu ndio mazingira anayopenda kuishi zaidi na katika kuthibitisha hilo anamiliki boti aina ya Hampshire II yenye urefu wa futi 260 ambayo thamani yake inatajwa kufikia Dola 150 milioni.

AT 05

MSAADA KWA JAMII

Ana taasisi iitwayo Jim Ratcliffe Foundation ambayo imejikita kwenye kusaidia jamii kwenye sketa mbalimbali ikiwamo afya na uchumi.

Aliwahi kuanzisha kampeni iliyoitwa "Go Run for Fun", ambayo ilikuwa na lengo la kukusanya pesa kwa ajili ya kusaidia watoto wenye umri wa kati ya miaka mitano hadi 10 ambao wana uhitaji.

AT 03

NDEGE NA MAGARI

Ana ndege tano na moja ikiwa ni helkopta, ndege hizo zote amekuwa akizutumia kwenye majukumu tofauti tofauti binafsi na kampuni. Jumla ya marubani 30 inadaiwa wameajiriwa kwa ajili ya ndege hizo.

Ndege hizo ni Gulfstream G650 (M-OVIE), Gulfstream G550 (M-USIC), Gulfstream G280 (M-ISTY), Gulfstream G280 (M-INTY) na Dassault Falcon 2000EX (M-CHEM)

Pesa zilizotumika kuzinunulia zinakadiriwa kufikia Dola 70 milioni.

Kwenye upande wa magari mara nyingi ameonekana akiendeshwa kwenye magari ya kampuni yake na BMW.

AT 02

BATA NA FAMILIA

Yupo kwenye ndoa na Maria Alessia Maresca ambaye alimuoa baada ya kuachana na Amanda Townson. Ana watoto watatu, wawili wa kiume na mmoja wa kike.

Anapenda sana kufanya utalii kwenye mbuga mbalimbali na mara nyingi anakuja kupumzika Afrika hasa Afrika ya Kusini.